Morgan Bahati ashindwa kuvumilia siku chache baada ya kupelekwa shule ya bweni, arudi nyumbani

Diana alisema huenda mambo yamekuwa magumu kwa Morgan shuleni kwa vile alikuwa amezoea maisha laini zaidi nyumbani.

Muhtasari

•Diana alidokeza kwamba mvulana huyo wa miaka 13 huenda alipata 'ugonjwa wa nyumbani' na kumfanya akose nyumbani.

•Diana alisema baada Morgan kulalamika, walimwendea shuleni, wakampeleka hospitali na kumruhusu apumzike nyumbani huku wakifuatilia hali yake.

MSANII BAHATI NA MWANAWE MORGAN BAHATI
Image: BAHATI/INSTAGRAM

Mwana wa kulea wa mwimbaji Kelvin ‘Bahati’ Kioko, Morgan Bahati amerejea nyumbani wiki chache tu baada ya kupelekwa katika shule ya msingi ya bweni.

Mke wa Bahati, Bi Diana Marua alifichua habari kuhusu kurejea kwa Morgan wakati wa kipindi cha vlog kwenye chaneli yake ya YouTube akidokeza kwamba mvulana huyo wa miaka 13 huenda alipata 'ugonjwa wa nyumbani' na kumfanya akose nyumbani.

Mwanablogu huyo alifichua kwamba mwanawe huyo wa kulea alipiga simu nyumbani na kulalamika kuhusu matatizo kadhaa ambayo alikumbana nayo tangu apelekwe kwenye bweni.

"Nyinyi nyote mnajua kuwa Morgan alienda kusoma katika shule ya bweni. Mnajua nini, yeye amerudi. Ametamani nyumbani," Diana Marua alifichua.

Aliongeza, "Alisema, "shule hii, mambo ni tofauti, mambo yamebadilika, nina shida ya tumbo, natapika, siwezi kubaki na chochote. Inafika mahali mpaka anasema ako na panic attack. Nikashangaa nini hii duniani!”

Mama huyo wa watoto watatu alidokeza kwamba huenda mambo yamekuwa magumu kwa Morgan shuleni kwa vile alikuwa amezoea maisha laini zaidi nyumbani.

“Unajua alikuwa amezoea ati anaamka, anaenda kutengeneza sossi cheese, bacon, noodles, alafu anakuja anaweka hapo anakula na anakunywa juice. Alafu anafungua friji anatoa ile kitu anataka.

“Huku alikuwa anaamka saaa nne, saa tano. Wakati wa shule anamka saa kumi na mbili unusu. Shule wanaamka saa kumi. Alipiga akasema ako na panic attack, hajiskii vizuri," mwanavlogu huyo alisema kwenye video.

Diana alisema kuwa baada ya kijana huyo wa miaka 13 kulalamika, walimwendea shuleni, wakampeleka hospitali na kumruhusu apumzike nyumbani huku wakifuatilia hali yake.

Morgan alijiunga na shule ya bweni mapema mwezi uliopita. Bahati alishiriki taarifa hizo kwa  kupitia kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii, zikiambatana na picha zake akiwa na Morgan akiwa amevalia sare za shule kikamilifu.

Iliyoambatana na picha hiyo ilikuwa barua ya moyoni kutoka kwa Bahati kwenda kwa mtoto wake ambapo bosi wa EMB records alisimulia nyakati ngumu alizopitia akiwa na Morgan, akitumaini kwamba wangemfanya Mungu ajivunie kwa baraka alizowapa.

“Mwanangu, Kuna Siku Tulizikosa, Kuna Siku ambazo Hatujatanguliwa, Kuna Siku tulililia fursa! Lakini Sasa kwa vile Baba Yetu wa Mbinguni Ametubariki na chakula, Nyumba na hata Nafasi ya Kupitia Maisha Ambayo Zamani yalikuwa Ndoto…. Ombi langu ni kwamba Tufanye Baba yetu wa Mbinguni Ajivunie… Fahari kwa Kutumia Fursa hii Aliyotubariki nayo,” alisema.

Aidha alimwambia afanye kazi kwa bidii ili alete matokeo mazuri nyumbani