Trevor aenda kinyume na msimamo wa awali kuhusu umiliki wa mitandao akitengana na Mungai Eve

Trevor alikuwa amesema katika tukio la bahati mbaya kwamba uhusiano wao ukiisha, angependelea Eve yeye abaki nayo.

Muhtasari

•"Huyu ni dame. Mi ndio najua. Mimi ndio nilicreate channel lakini ni yake," Trevor alisema kabla ya kurudia vivyo hivyo kwa mara nyingine tena.

•Kauli ya Trevor inakwenda kinyume na alichokifanya sasa kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kuhusu kutofanya kazi tena na Eve.

Director Trevor wakiwa na mchumba wake Mungai Eve Picha/Instagram
Director Trevor wakiwa na mchumba wake Mungai Eve Picha/Instagram
Image: HISANI

Kama wengi wenu mnafahamu vyema hivi sasa, mtaakamu wa mitandao ya kijamii Director Trevor ametangaza kuwa hatafanya kazi tena na mpenzi wake wa muda mrefu Mungai Eve.

Wachambuzi wengi wajanja watakuambia, habari ni ishara kwamba mambo sio sawa kabisa kati ya wawili hao na kuna uwezekano mkubwa kwamba tayari wameachana

Lakini kama ilivyo kawaida yetu nchini Kenya, wanamitandao wamefufua video ya kumbukumbu ambapo Trevor anazungumzia suala la kuachana na mpenzi wake maarufu zaidi.

Katika video hiyo ya mahojiano ya zamani na Mwanahabari mwenzake wa YouTube, Presenter Ali alikuwa ameulizwa jinsi uhusiano wao wa kikazi ungeendelea ikizingatiwa kuwa Eve ndiye aliyekuwa mhoji huku Trevor akipiga video hizo.

Eve alicheka kwa wasiwasi huku Trevor akiendelea kuzungumzia hali hiyo ya kutatanisha, akisema

"Huyu ni dame. Mi ndio najua," alisema huku kukiwa na vicheko kati ya wale watatu kabla ya kuendelea kusema, "Mimi ndio nilicreate channel lakini ni yake," kabla ya kurudia vivyo hivyo kwa mara nyingine tena.

Kisha akaongeza kuwa katika tukio la bahati mbaya kwamba uhusiano wao umeisha, angependelea yeye abaki nayo.

"Labda kukiwa na masuala ningepends iwe yake. Mimi naeza anza channel leo na bado iwe freshi kabisa.

Kwa sababu brand ni yake, jina ni lake. Hata saa hii habari zote ni zake. Mimi najua tu password. Mambo mengine sijui. Mambo ya hela sijui."

Kauli ya Trevor hapo juu inakwenda kinyume na alichokifanya sasa kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kuhusu kutofanya kazi tena na Eve.

Si hivyo tu, pia alisema kuwa atakuwa akibadilisha majina ya chaneli maarufu kuwa jina jipya la chapa.

Je, nini kingetokea kwa yeye kurejea ahadi aliyoitoa kwenye mahojiano ya zamani? Nadhani yako ni nzuri kama yangu.