Inapendeza! Binti wa Harmonize na bintiye wa kambo waonyesha uhusiano mzuri

Konde Boy amewasherehekea wasichana hao wadogo huku akijitambua yeye na mpenzi wake kama wazazi wanaowajibika.

Muhtasari

•Konde Boy ana binti wa miaka mitano na mfanyabiashara wa Tanzania Official Leen huku Poshy Queen pia akiwa na mtoto mmoja.

•Mwanasosholaiti Poshy Queen alitumia fursa hiyo kueleza upenda walionao wasichana hao wawili kwa baba yao Harmonize.

Harmonize na mpenzi wake Poshy QUEEN
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize na mpenzi wake Poshy Queen wameshiriki video nzuri ya binti wao wakicheza pamoja.

Konde Boy ana binti wa miaka mitano na mfanyabiashara wa Tanzania Official Leen huku Poshy Queen pia akiwa na mtoto mmoja ambaye alipata na mpenzi wake wa zamani wa Nigeria.

Katika video ambayo wapenzi hao walichapisha kwenye kurasa zao Ijumaa, bintiye Harmonize, Zuuh Konde na bintiye Poshy Queen Nova walionekana wakichora pamoja huku wakionyesha uhusiano mzuri sana kati yao. Wawili hao walionekana kufurahia kucheza pamoja.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alitumia fursa hiyo kuwasherehekea wasichana hao wawili huku akijitambua yeye na mpenzi wake kama wazazi wanaowajibika.

“Tunawajibika rafiki yangu @poshyqueen. Kheri ya siku ya kimataifa ya wanawake wasichana wangu,” aliandika Harmonize.

Kwa upande wake, mwanasosholaiti Poshy Queen alitumia fursa hiyo kueleza upenda walionao wasichana hao wawili kwa baba yao Harmonize.

Staa huyo wa bongo fleva na Poshy Queen wamekuwa wakichumbiana kwa muda sasa na hawajaona haya kuonyesha mapenzi yao hadharani.

Mapema mwaka huu, Konde Boy alidokeza kuwa uhusiano wake mpya hauhusishi kuficha mambo yoyote akifichua kuwa mwanamke anayechumbiana naye huwa na simu yake wakati mwingine.

"Mwanaume mwaminifu ulimwenguni! Mpenzi wangu huenda na simu yangu ya rununu, tayari ana password ya simu yangu. Iwapo utapata jibu lisilo la kawaida, bado nina upendo nanyi nyote,” alisema Harmonize kupitia Instastories yake.

Mwanamuziki huyo alifichua kuwa alitaka kuchumbuina na mpenzi wake kitambo lakini uhusiano wao haukufaulu wakati huo kama walivyokusudia.

Aidha, aliendelea kutangaza kuwa sasa ametulia kwani mwanamke anayetoka naye sasa hivi atakuwa wa kudumu kwake.

“Hapa ndio mwisho wangu. Onyoo, hajawahi kutembea na yeyote ninayemjua. Mheshimu kama msichana wangu. Popote utakapomuona uache drama!” alisema