Mrembo alilia haki bosi kumkata 4,800 kutoka kwa mshahara wa 5,400 akidai anazembe kazini

Kwa mujibu wa kesi hiyo ya kusikitisha iliyochapishwa mtandaoni X, mrembo huyo ambaye ameandikwa kazi kwenye biashara ya uchuuzi alikatwa pesa hizo na kulipwa Ksh600 pekee baada ya mteja ku'reverse pesa alizolipia huduma.

Muhtasari

• Mwishoni mwa mwezi, mrembo huyo alipigwa na butwaa kulipwa tu N6000, sawa na Ksh 600 akiambiwa zingine zilikatwa kufidia makosa ya mteja aliyerudisha pesa baada ya malipo.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Mwanamke mmoja ameomba usaidizi mitandaoni baada ya kudai kutendwa na mwajiri wake aliyedai alimkata kiasi kikubwa cha mshahara wake wa mwezi.

Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa X na mtumizi kwa jina Foundational Nupe Lawyer1, mrembo huyo alikuwa ameandikwa kazi mshahara wa kila mwezi ukiwa N59,000 za Nigeria sawa na 5400 za Kenya.

Lakini baada ya kumuuzia mteja mmoja ambaye alikubali kulipa kwa njia ya simu na baadae akarudisha zile pesa, bosi alighadhabika akidai mrembo huyo alizembea kazini hivyo kumtaka N53,000 sawa na Ksh 4,800 kufidia hasara hiyo.

Mwishoni mwa mwezi, mrembo huyo alipigwa na butwaa kulipwa tu N6000, sawa na Ksh 600 akiambiwa zingine zilikatwa kufidia makosa ya mteja aliyerudisha pesa baada ya malipo.

Kwa maneno yake: "Jana, mwanamke alinililia kwamba mwajiri wake alikatwa 53k kutoka kwa mshahara wake na kumlipa 6k kwa mwezi kwa sababu pesa za mteja zilirudishwa”.

Lakini Je, mwajiri anaweza kukata kwenye mshahara wako?

Kuzungumza kisheria, kwa ujumla, hakuna mwajiri aliye na haki yoyote ya kukata kiasi chochote kutoka kwa mishahara uliyokubali isipokuwa makato yanayoruhusiwa na sheria, kama vile kodi, pensheni na makato mengine ya kisheria.

Tazama chapisho hapa chini: