Ex wa Baha, Georgina Njenga afunguka kuhusu kuchumbiana tena

Mtayarishaji maudhui Georgina Njenga amefunguka kuhusu mipango ya kuingia katika mahusiano mengine.

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya alizungumza kuhusu kuchumbiana tena alipokuwa akimjibu shabiki aliyekiri kumpenda.

•Alibainisha kwamba wakati pekee ambao atakuwa tayari kuchumbiana tena ni wakati Mungu Mwenyewe atakapomwelekeza.

Image: INSTAGRAM// TYLER MBAYA

Mtayarishaji wa maudhui Georgina Njenga amefunguka kuhusu mipango ya kuingia katika mahusiano mengine.

Mpenzi huyo wa zamani wa muigizaji Tyler Mbaya almaarufu Baha alizungumza kuhusu kuchumbiana tena wakati alipokuwa akimjibu shabiki aliyekiri kumpenda.

“Nakutakaaa,” shabiki mmoja alimwandikia kwenye Instagram.

Katika majibu yake, mama huyo wa binti mmoja aliweka wazi kuwa kwa sasa hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano mengine.

Alibainisha kwamba wakati pekee ambao atakuwa tayari kuchumbiana tena ni wakati Mungu Mwenyewe atakapomwelekeza.

"Sichumbiani tena hadi Mungu Mwenyewe atakapokuja na kuketi juu ya kitanda changu na kusema, 'Mmoja wa vijana wangu wa nyumbani anataka kuzungumza nawe!," Georgina alijibu.

Mtayarishaji maudhui huyo mrembo mwenye umri wa miaka 23 amejaribu kuweka maisha yake ya mahusiano kuwa ya faragha kwa muda mrefu sasa, hasa baada ya kuthibitisha kutengana kwake na muigizaji Baha katikati ya mwaka jana.

Mwezi Julai mwaka jana, mama huyo wa binti mmoja alithibitisha kutengana na muigizaji wa zamani wa Machachari Tyler Mbaya almaarufu Baha.

Mapema mwaka huu, mtayarishaji huyo wa maudhui aliweka wazi kuwa yeye bado hana mpenzi lakini hatafuti.

Alifichua hayo wakati wa mahojiano na mwanahabari Nicholas Kioko baada ya kuhojiwa kuhusu hali ya uhusiano wa  ex wakeTyler Mbaya. Alibainisha kuwa hawezi kujua ikiwa mzazi mwenzake, Tyler Mbaya amesonga mbele na maisha yake au la, lakini pia akathibitisha kuwa yeye yuko peke yake lakini hatafuti mpenzi.

"Sijui kama amemove on lakini mimi niko soko...bado sijapata mpenzi lakini sitafuti... Niko soko kujitafuta, na kugrow," alisema.

Alisema zaidi kwamba alitamani maisha yake na baba ya mtoto wake.

"Ndio kweli lakini maisha yalitokea, mambo yalitokea hivyo tunaendelea. Kitu kimoja cha maisha ni maisha yanasonga mbele, maisha yanaendelea hivyo hata nikimmiss, hizo ni kumbukumbu na angalau Astara atakua anasema tulikuwepo."

Georgina pia alifichua kwamba mipango ya baadaye ya uhusiano wake na Tyler haijulikani lakini akabainisha kuwa sura hiyo haikufungwa kabisa.

"Nadhani ningesema hujui na maisha. Huwezi pangia maisha. Leo naeza kuwa nimepanga kuwa hatutarudiana alafu turudiane ama niseme hapa hatuezi rudiana nayeye alafu turudiane. Ama niseme tunaeza rudiana alafu tukose. But of cause, destiny holds its place so maybe its place so maybe rudiana nayeye alafu turudiane. siku moja.

Kama vile sina mpango kuhusu maisha yangu. Nita panga ndio lakini Mungu ndio ako na ufunguo mkuu kwa hivyo labda ndio, labda hapana, lakini ni kitu ambacho sijafunga kabisa kutoka kwa sura yangu," Georgina alisema.