“Mpenzi aliniacha na kuendea msichana ambaye pia ex wangu alinibadili naye!” – Mrembo alia

Alieleza jinsi alivyoumia moyo baada ya kugundua kwamba mpenzi wake alimuacha na kuanza kuchumbiana na msichana yule yule ambaye mpenzi wake wa zamani pia alimuacha na kuanza kuchumbiana naye.

Muhtasari

• "Natweet kwa sababu maisha hayakuisha wakati ex wangu aliniacha na kwenda kwa msichana yuleyule ex wangu mwingine aliniacha na kumuendea 🤭"

• Kutokana na ungao hilo, Watumizi wa Twitter walitoa maoni mbalimbali, wengine wakimpa ushauri wa ajabu.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Kipusa mmoja amechukua kwenye mtandao wa X kuelezea mafadhaiko yake kuhusu kile anachokihisi kuwa ni kuwa na nuksi katika mapenzi.

Kwa mujibu wa mrembo huyo, alieleza kwa uchungu jinsi amekuwa na gundu katika uwanja wa mapenzi, huku wapenzi wake kila mara wanapomuacha, wote huishia kuchumbiana na msichana mmoja tu.

Msichana huyo kwa jina la utambulisho @Rukkyjunaid alitoa simulizi yake akijibu ujumbe wa Twitter uliokuwa ukiwauliza watu kusimulia tukio lililowafanya wahisi kama maisha yanawageuka na kuwaendea kombo.

Alieleza jinsi alivyoumia moyo baada ya kugundua kwamba mpenzi wake alimuacha na kuanza kuchumbiana na msichana yule yule ambaye mpenzi wake wa zamani pia alimuacha na kuanza kuchumbiana naye.

Kulingana na mwanamke huyo, uhusiano wake wa kwanza ulivunjika baada ya mpenzi wake kumwacha na kumfuata mwanamke mwingine.

Alianza uhusiano na mvulana mwingine ambaye hatimaye alimwacha na kumfuata mwanamke huyo huyo.

@Rukkyjunaid alisema:

"Natweet kwa sababu maisha hayakuisha wakati ex wangu aliniacha na kwenda kwa msichana yuleyule ex wangu mwingine aliniacha na kumuendea 🤭"

Kutokana na ungao hilo, Watumizi wa Twitter walitoa maoni mbalimbali, wengine wakimpa ushauri wa ajabu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumizi wa X;

“Umewahi fikiria labda kuungana na huyo msichana ili kujua chanzo cha wapenzi wako kutumbukia katika kapu lake ni lipi?” Ayo, the First alimuuliza.

“Unapoteza nyumbani na mbali na mbali na nyumbani,” Abolaji.

“Uko chini kwa mabao 2-0, lazima utoke nje” Sheddy.

“Hapo mimi itanibidi nijumuishe watu wangu wa kijijini kufanya mambo,” Oloris.

Tazama Tweet yake na utoe maoni yako: