Babu Owino akanusha kulipiwa dhamana na Johnson Sakaja wakati alishikwa

“Acha kudanganya Wakenya Sakaja Johnson. Ulikuja kwenye kituo cha polisi cha Parklands kutafuta kiki ya kisiasa. Nililipa dhamana yangu ya pesa taslimu ya 100k" Babu alisema.

Muhtasari

• “Kazi yangu ya kuwaleta watu pamoja haijaanza hivi majuzi. Babu Owino alipokamatwa nani alimdhamini? Ninaamini katika Nairobi moja."

• Babu Owino aliyekasirishwa alijibu kwenye X (zamani Twitter) akidai Sakaja alikuwa anawadanganya Wakenya tena.

Mzozo umeibuka upya kati ya mbunge wa Embakasi East Babu Owino na gavana wa jiji Johnson Sakaja.

Hii ni baada ya Sakaja kudai kwamba wakati mbunge huyo alishikwa na polisi, yeye ndiye alikwenda na kumtoa ndani kwa kumlipia dhamana.

Mnamo Jumatano, Gavana Sakaja katika hotuba yake katika eneo la Bomas of Kenya alidai kuwa amemtoa mbunge Babu Owino kutoka seli za polisi.

“Kazi yangu ya kuwaleta watu pamoja haijaanza hivi majuzi. Babu Owino alipokamatwa nani alimdhamini? Ninaamini katika Nairobi moja."

Babu Owino aliyekasirishwa alijibu kwenye X (zamani Twitter) akidai Sakaja alikuwa anawadanganya Wakenya tena.

“Acha kudanganya Wakenya Sakaja Johnson. Ulikuja kwenye kituo cha polisi cha Parklands kutafuta kiki ya kisiasa. Nililipa dhamana yangu ya pesa taslimu ya 100k. Nimekamatwa mara nyingi sana na bado unaweza kuniona karibu, unataka kusema kwamba umekuwa ukinisaidia katika kesi zangu?" alisema.

Saa mbili baadaye, Owino alishiriki kipande cha video kinachoonyesha kundi linalodaiwa kuwa la wafanyikazi wa Kaunti ya Nairobi katika maandamano wakiimba “Sakaja lazima aondoke!”

“Mambo imechemka kwani wafanyikazi wa kaunti ya Nairobi wamechoshwa. (Mambo yanachemka huku wafanyikazi wa Kaunti ya Nairobi wamechoshwa),” mbunge huyo aliandika.

Hapo awali, mkuu huyo wa kaunti alitishia kuwafuta kazi baadhi ya wafanyikazi wake kwa madai kuwa wanadharau uongozi wake.