Wakili wa kike aoana na mume wa mwanamke aliyemsaidia kufanikisha talaka mahakamani

Baadhi walimtetea wakisema kuwa kando na kuwa wakili, yeye ni binadamu na anahitaji mapenzi hivyo kuoleka kwa aliyekuwa mume wa mteja wake ni sahihi kwani alijua si mume wa mtu tena baada ya talaka.

Muhtasari

• Hili lilivutia maoni mseto, baadhi wakidai kwamba katika kizazi cha sasa, mtu hufai kumuamini mtu yeyote hata kama ni mzazi au ndugu yakow a toka nitoke.

Mume amuacha mkewe siku mbili baada ya kufunga harusi kisa alipigania chakula na mamake siku ya harusi.
Mume amuacha mkewe siku mbili baada ya kufunga harusi kisa alipigania chakula na mamake siku ya harusi.
Image: BBC NEWS

Mwanamke mmoja amechukua kwenye mtandao wa kijamii kuonyesha kuchanganyikiwa kwake baada ya kugundua kwamba wakili wake ambaye ni wa kike sasa ameoana na mume wake ambaye wakili huyo alimsaidia kufanikisha talaka mahakamani.

Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ilirejelewa na mtumizi mmoja wa mtandao wa Facebook kwa jina la Ojong Agbor, aliripoti kwamba mwanamke huyo alifadhaika pakubwa baada ya kubaini hilo, wiki mbili baada ya mchakato wa kesi yao ya talaka kupata mwafaka mahakamani.

Mwanamke huyo kwa kuchanganyikiwa na kufadhaika kwa viwango sawa, alilia kwamba baada ya mng’ang’ano wa kesi yake ya kutaka kuachana na mume wake, kesi ambayo alisaidiwa na wakili wa kike, wiki mbili baadae amegundua wakili huyo ndiye amerithi nafasi yake kama mke wa mume wake wa zamani ambaye wametalikiana.

“Wakili aliyenisaidia kushughulikia kesi yangu ya kutalikiana na mume wangu sasa ameoana na aliyekuwa mume wangu, wiki mbili baada ya kukamilika kwa mchakato wa kesi ya talaka mahakamani,” Agbor alimnukuu mwanamke huyo.

Hili lilivutia maoni mseto, baadhi wakidai kwamba katika kizazi cha sasa, mtu hufai kumuamini mtu yeyote hata kama ni mzazi au ndugu yakow a toka nitoke.

Hata hivyo, baadhi walimtetea wakili huyo wakisema kuwa kando na kuwa wakili, bado yeye ni binadamu tu ambaye anahitaji mapenzi na kukubali kuoleka kwa aliyekuwa mume wa mteja wake ni sahihi kwani alijua vizuri kwamba si mume wa mtu tena bali ni mume huru baada ya kutalikiwa.

Tazama chapisho hilo hapa na utoe maoni yako;