Mchungaji Kanyari asema hayupo TikTok kupata pesa bali kuokoa nafsi

"Siko pale ili kupata pesa tu lakini watu waokolewa, sio kwa pesa," alisema.

Muhtasari

•Mchungaji Kanyari alieleza kuwa alikuwa kwenye TikTok kuhubiri injili hili watu waokoke, kinyume na watu wengi wanaamini.

•Baadhi ya wanamtandao hawakukubaliana naye na kujiuliza ni lini aliwahi kuhubiri kwenye TikTok, huku wengine wakihoji iwapo waumini wake hawakuwa kwenye programu ya mitandao ya kijamii.

Pastor Kanyari
Pastor Kanyari
Image: HISANI

Mhubiri mashuhuri Mchungaji Victor Kanyari ameweka mambo wazi kuhusu kwa nini anashiriki sana TikTok ikilinganishwa na watu wengine wa Mungu.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mtu wa Mungu aliwaambia washiriki wa kanisa lake wasijiunge na TikTok kwa sababu wangekasirishwa na watumiaji wa mtandao wanaomkashifu.

Kanyari pia alieleza kuwa hana nia ya kutafuta pesa licha ya watu kumtumia zawadi kila mara kwenye programu hio ya kijamii.

Mchungaji Kanyari pia alieleza kuwa alikuwa kwenye TikTok kuhubiri injili hili watu waokoke, kinyume na watu wengi wanaamini.

"Tunataka kubaki kwenye TikTok ili tujaribu kuokoa watu ili waweze kumpenda Yesu.

Hatupo kwa ajili ya pesa tu, ingawa watu hunitumia pesa, na huwa nashangaa.

Siko  pale ili kupata pesa tu lakini watu waokolewa, sio kwa pesa," alisema.

 Pia aliapa kuendelea kupigana na watu kwenye TikTok huku akiwauliza waumini wake tu kufuata kile kinachotokea kanisani lakini wasifuatilie mambo ya mtandao.

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii:

@Desmond:

"It's how he moves from Kufinish Kumalo to Bwana asifiwe. Wewe hupreach lini?"

@Happiness Abby:

"But pastor sijaona ukihubiri TikTok."

@matonimoses :

"But Kanyari is the one who needs deliverance."

@Fruitful tree:

"I usually wonder what is going on in their minds when sitting done there."

@kulu:

"Sema tu ukweli hutaki waone vituko unafanya huko TikTok."