Otesa arejea Bungoma baada ya kukosa kukutana na Gen Z Mtall

Isaac Otesa amerudi nyumbani Bungoma wiki chache baada ya Manzi wa Kibera kumualika Nairobi

Muhtasari

•Isaac Otesa amerudi nyumbani Bungoma wiki chache baada ya Manzi wa Kibera kumualika Nairobi

•Alikuja Nairobi na matarajio ya kupatana na Bradley lakini hawakukutana

Isaac Otesa
Image: HISANI

Isaac Otesa a.k.a Bungoma Goliath amerudi nyumbani wiki chache baada ya Manzi wa Kibera kumualika Nairobi.

Kulingana na video iliyowekwa mtandaoni, Otesa alionekana Bungoma na mkoba wake.

Mashabiki wanasema kuwa maisha yake haijabadilika isipokuwa mtindo wake wa kuvaa wengine wakimuonea huruma kuwa alikuja mjini na bado hakupata umaarufu kama alivyotarajia.

Otesa alisafiri kuja Nairobi Agosti, akitarajia kukutana na Bradley ambaye anadai ni ndugu yake. Hata hivyo hawakukutana.

Katika mahojiano, Otesa alisema kuwa yeye ni mrefu kumliko Bradley sababu ikiwa yeye ana urefu wa futi 8.4 mwenzake akiwa na urefu futi 8.2.

Katika akaunti ya Tiktok wa Manzi wa Kibera, meneja wake amesema kuwa Isaac ameenda nyumbani kuona bibi yake. Anasema kuwa Isaac amenda kuona bibi kwani ana mtoto wa miezi 1 na wiki 1 lakini atarudi hivi karibuni.

"Isaac, Goliath wa Bungoma amerudi ushago, naona watu wanasema Manzi wa Kibera ameshindwa kufanya kazi na yeye..lakini unajua Isaac ameoa na ana mtoto. Mtoto wake ana kama mwezi 1 wiki 1 hivyo ni lazima arudi nyumbani. Na atarudi hivi karibuni kwa sababu ana  dili kubwa sana ambazo zitashangaza watu wengi...basi tuache kumdharau Isaac. At the end of the day, hakuchagua kuwa mrefu ama kufanana na Bradley...Isaac amerudi ushago but amerudi kuona wife," chali wa Kibera alisema.