Nilipomaliza sekondari mwalimu wa math alitaka twende tujivinjari - Elsa Majimbo

"Alinitumia huu ujumbe mrefu ambapo aliniambia jinsi alivyoniona mrembo na kuwa alidhani tuna uhusiano na tunafaa kuonana ili twende date," Majimbo alisema.

Muhtasari

•Elsa Majimbo afichua kuwa alipomaliza shule ya upili mwalimu wake wa hisabati alimtumia ujumbe waende wajivinjari pamoja

Image: INSTAGRAM// ELSA MAJIMBO

Mchekeshaji Elsa Majimbo amefichua kuwa alipomaliza shule ya upili mwalimu wake wa hisabati alimtumia ujumbe waende wajivinjari pamoja.

Kwa video aliyochapisha TikTok, Majimbo anasema kuwa alimaliza shule akiwa na umri wa miaka 17 na mwalimu wake alimtumia ujumbe mrefu akimwambia kuwa yeye ni mrembo na wanafaa kukutana ili waende kujivinjari pamoja.

“Mara tu nilipomaliza shule ya upili, mwalimu wangu wa hesabu aliniuliza twende tujivinjari. Nilimaliza shule ya upili  nikiwa na miaka 17. Alinitumia huu ujumbe mrefu ambapo aliniambia jinsi alivyoniona mrembo na kuwa alidhani tuna uhusiano na tunafaa kuonana ili twende date," Majimbo alisema.

Alisema kuwa hajawai mwambia mtu yeyote na kuwa hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kwani wakati huo alimwambia rafiki yake mmoja ambaye alishauri asimwambie yeyote.

“Sikuwahi kumwambia mtu yeyote kuhusu hili jambo. Nilimwambia rafiki yangu mmoja ambaye alininiambia ‘ooh he’s a good guy..don’t tell anyone,'

Majimbo anasema kuwa hilo sio jambo la kawaida na kuwashauri mashabiki wake kushtaki mambo kama hayo.

“If your teacher hits on you or If you feel like there’s some sort of thing that’s going on that’s not right , snitch snitch. I wish I had snitched coz I’m sure he did that to someone else like I couldn’t have been the last one or first one,” alisema.