"Awali alionekana kuchanganyikiwa!" Gidi afichua jinsi mke wa Bobi Wine amembadilisha

Gidi alibainisha kuwa Barbie amekuwa nguzo kubwa katika maisha ya Bobi Wine.

Muhtasari

•Gidi amezungumzia jinsi anavyopendezwa na wanandoa Bobi Wine na mke wake Barbara Kyagulanyi almaarufu Barbie.

•Kufuatia hayo, mtangazaji huyo amewashauri wanaume kuoa wanawake wanaoungana nao na wanaoamini katika ndoto zao.

amekiri kufurahishwa na ndoa ya Bobi Wine na Barbie
Gidi amekiri kufurahishwa na ndoa ya Bobi Wine na Barbie
Image: INSTAGRAM

Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, Joseph Ogidi almaarufu Gidi amezungumzia jinsi anavyopendezwa na ndoa ya Bobi Wine na mke wake Barbara Kyagulanyi almaarufu Barbie.

Katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook, mtangazaji huyo alibainisha kuwa Barbie amekuwa nguzo kubwa katika maisha ya mwimbaji na mwanasiasa huyo wa Uganda.

Gidi alisema mama huyo wa watoto wanne amekuwa akisimama na Bobi Wine siku zote na kubainisha kuwa ameendelea sana tangu alipokutana naye mara ya kwanza.

"Nimetoka kutazama mahojiano kwenye Sky News, ambapo mke wa Bobi Barbie anaelezea masuala ya Uganda katika jukwaa la kimataifa kwa uangalifu sana. Alikuwa mdogo sana nilipokutana naye kwa mara ya kwanza. Nilichokiona leo ni mabadiliko makubwa. Amesimama na Bobi miaka yote hiyo na ninaamini ndiye msukumo wa safari ya kisiasa ya Bobi Wine. Wale waliomjua Bobi Wine kabla ya mabadiliko haya watakubaliana nami,” Gidi alisema siku ya Jumatano.

Mwimbaji huyo wa zamani wa bendi ya Gidi Gidi Maji Maji pia alifichua kuwa Bobi Wine siku zote alionekana kukosa mwelekeo kuliko waimbaji wenzake wa Uganda, Chameleone na Bebe Cool walipokuwa wakitembelea jijini Nairobi miaka mingi iliyopita, hali ambayo sasa imebadilika.

Aidha, alibainisha kuwa mkewe Wine amekuwa na jukumu kubwa la kucheza katika mabadiliko makubwa ya tabia na mwelekeo wake wa maisha..

“Bobi Wine, Chameleon na Bebe Cool na wasanii wakubwa wa Uganda, walikuwa wageni wa mara kwa mara nyumbani kwangu Nairobi miaka mingi iliyopita tulipokuwa tungali na bidii katika muziki. Kitu kimoja nilichoona nikiwa na Bobi wakati huo alionekana kuchanganyikiwa sana kati ya wale watatu,” alisema.

Kufuatia hayo, mtangazaji huyo mahiri amewashauri wanaume kuoa wanawake wanaoungana nao na wanaoamini katika ndoto zao.

"Oa aina yako, uoe muumini wako, uoe mshangiliaji wako. Rafiki yangu mwingine wa zamani wa UG ni Dave Kazoora maoni yenu ni yapi, tumekuwa hapo na tumefanyah hayo," Gidi aliandika.

Bobi Wine amekuwa akiishi na Barbie kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Wawili hao walifunga ndoa mwaka wa 2011 na wamejaliwa watoto wanne pamoja