Bahati, Diana Marua waeleza jinsi tendo la ndoa ni muhimu katika kudumisha ndoa yenye furaha

Mwimbaji huyo alibainisha kuwa tendo la ndoa pia husaidia katika kutatua mizozo katika ndoa.

Muhtasari

•Bahati aliwataka wanandoa kuchukua ngono kwa uzito ikiwa wanataka kuwa katika ndoa yenye furaha na akawaonya dhidi ya kuwa na ubinafsi nayo.

•Diana aliwashauri wapendanao kuwa marafiki kwanza na kuelewana vizuri ili kuwa na ndoa ya kudumu na yenye furaha.

Diana Marua na Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Wanandoa maarufu wa Kenya, Kelvin ‘Bahati’ Kioko na Diana Marua wamefichua kuwa tendo la ndoa ni kipengele muhimu sana katika ndoa.

Wanandoa hao walikuwa wakimjibu shabiki aliyeuliza kuhusu siri ya ndoa yenye mafanikio walipozungumzia thamani ya mchezo huo wa kitandani.

Bahati aliwataka wanandoa kuchukua ngono kwa uzito ikiwa wanataka kuwa katika ndoa yenye furaha na akawaonya dhidi ya kuwa na ubinafsi nayo.

"Kwa ndoa yenye furaha iliyofanikiwa, jambo la kwanza, chukua tendo la ndoa kama mkate wa kila siku. Kwa ndoa yenye mafanikio, hakuna njia unaweza kuwa mchoyo nalo,” Bahati alisema wakati wa kipindi cha uwazi kwenye chaneli ya YouTube ya Diana Marua.

Diana Marua alionekana kukubaliana kabisa na mume wake kuhusu umuhimu wa tendo la ndoa katika kudumisha ndoa yenye furaha.

Bahati aliendelea kuwaonya wapenzi dhidi ya kuwanyima wapenzi wao mapenzi, akidokeza kuwa hiyo ndiyo sababu ya watu kuachana.

“Ukipeana hizo vitu vingine zitajileta. Kama Bibilia inavyosema, Utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake yote, na hayo mengine yote mtazidishiwa. Tendo la ndoa ni ufalme katika ndoa,” Bahati alisema.

Mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili alibainisha kuwa tendo la ndoa pia husaidia katika kutatua mizozo katika ndoa. Pia alisisitiza kumkumbatia Mungu katika ndoa.

Diana aliwashauri wapendanao kuwa marafiki kwanza na kuelewana vizuri ili kuwa na ndoa ya kudumu na yenye furaha.

"Kuweni marafiki kwanza na pili elewa kuwa nyinyi ni binadamu wawili tofauti, jifunzeni kuhudumiana," alisema.

Mama huyo wa watoto watatu alibainisha kuwa kumwelewa mwenzi wako na kujifunza jinsi ya kukabiliana naye husaidia katika kutatua migogoro.