Dadake Diamond alalamikia Wakristo wengi kutembelea Waislamu wakati wa mlo wa Iftar

."Kila nyumba ninayoiyona wakristo wanataradadi na kanzu zao," Esma alisema.

Muhtasari

•Esma alisema kuwa amebaini kwamba vikao vingi ya Iftar alivyohudhuria, wengi wamekuwa Wakristo waliovalia mavazi ya Kiislamu.

•Mwezi uliopita, Esma  alizamia kwenye Instagram kuwaomba msamaha wanafamilia wake kabla ya mwezi wa Ramadan kuanz

Esma Platnumz na Diamond
Image: HISANI

Dada mkubwa wa mwimbaji wa Bongo Diamond, Esma Platnumz ameibua wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya Wakristo wanaotembelea nyumba za Waislamu wakati wa milo ya Iftar katika msimu wa Ramadhani wa mwaka huu.

Katika chapisho kwenye ukurasa wake, mfanyibiashara huyo wa nguo alisema kuwa amebaini kwamba katika vikao vingi ya Iftar alivyohudhuria tangu Ramadhan kuanza, wengi wamekuwa Wakristo waliovalia mavazi ya Kiislamu.

"Maisha haya mwaka huu wanaoongoza kufturishwa ni Wakristo. Kila nyumba ninayoiyona wakristo wanataradadi na kanzu zao," Esma Platnumz alisema kwa mzaha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Utakuta mduara  wa watu kumi, Muislamu mmoja, wote Wakristo na vilemba vyao."

Kwa wasio na habari, Iftar ni mlo wa kufungua mfungo wa kila siku katika mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani.  Mwaka huu, Waislamu wengi kote duniani walianza kuadhimisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani mnamo tarehe 22 Machi na wanatarajiwa kuufunga tarehe 20 Aprili, 2023.

Kauli ya mama huyo wa watoto watatu inakuja wakati Wakristo kote duniani wanasherehekea Pasaka. Huku akiwatania Wakristo, Esma Platnumz alidokeza kwamba sio wengi ambao wanajua kupika Biriani.

"Wakristo mnavyozima simu, utadhani mnaweza kupika Biriani," alisema kupitia meme.

afanya sala huku mwezi wa Ramadani ukiendelea
Diamond afanya sala huku mwezi wa Ramadani ukiendelea
Image: INSTAGRAM

Mwezi uliopita, Esma  alizamia kwenye Instagram kuwaomba msamaha wanafamilia wake kabla ya mwezi wa Ramadan kuanza. Hatua hiyo ilikabiliwa na utata kwani ilikuja siku chache baada ya kujirekodi akiimba wimbo wa Harmonize.

Akizungumza kwenye mahojiano ya hivi majuzi na Wasafi Media, dada huyo wa Diamond hata hivyo aliweka wazi kwamba hakuchukua hatua hiyo kwa sababu ya video yake ila kwa ajili ya mwezi wa Ramadan.

"Mimi sikuomba ndugu zangu msamaha. Nimeomba watu wengi, marafiki na hata wateja wangu. Nimeomba msamaha kwa sababu ya Ramadan. Mimi na ndugu zangu hatuna tatizo lolote," Esma alisema.

Esma aliweka wazi kwamba yeye kawaida hucheza nyimbo za wasanii wengi wa Bongo  bila upendeleo, jambo ambalo wanafamilia wake wanafahamu.

"Huwa naimba nyimbo za Alikiba, naimba za Marioo,naimba nyimbo za Harmonize. Sijaona kitu kibaya kwetu na hamna mtu aliyenikasirikia," alisema.

Mfanyibiashara huyo pia alizika tetesi kwamba uhusiano wake na Mama Dangote uliathirika baada ya kurekodi video hiyo.

"Mimi na familia yangu asilimia 100 tuko vizuri. Mamangu siku zote hawezi kugombana na mimi. Mimi ndiye mtoto wangu pendwa. Mimi na mama hatujawahi kukoseana, mimi na familia yangu sijawahi kuikosea," alisema.