Karen Nyamu ajibu kwa nini huwa hamuonyeshi baba mtoto wake wa kwanza kama Samidoh

"Na kwa nini huwa hupost baba mtoto wako wa kwanza?" Karen Nyamu aliulizwa.

Muhtasari

•Karen Nyamu alilazimika kueleza kwa nini huwa hamuonyeshi baba wa mtoto wake wa kwanza kama anavyomuonyesha Samidoh.

•Mcheza santuri wa Kenya, DJ Saint ndiye baba wa mtoto wa kwanza wa Karen Nyamu. 

Karen Nyamu na mzazi mwenzake DJ Saint Kevin
Image: HISANI

Siku ya Jumanne, seneta Karen Nyamu alilazimika kueleza kwa nini huwa hamuonyeshi baba wa mtoto wake wa kwanza kama anavyojigamba kuhusu baba watoto wake wawili wa mwisho, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Katika akaunti zake za mitandao ya kijamii, mama huyo wa watoto watatu alionyesha video na picha kadhaa baada ya kuhudhuria hafla ya Siku ya Michezo katika shule ya mwanawe, Sam Jr pamoja na mzazi mwenzake Samidoh.

Chini ya picha hizo, shabiki mmoja alitaka kujua kwa nini seneta huyo hafanyi sawa na mzazi mwenzake mwingine, DJ Saint.

"Na kwa nini huwa hupost baba mtoto wako wa kwanza?" mtumizi wa Instagram alimuuliza.

Seneta Nyamu kwa utani alijibu, "Kwani watu hupost ex zao."

Mcheza santuri wa Kenya, DJ Saint ndiye baba wa mtoto wa kwanza wa Karen Nyamu. Wawili hao walichumbiana kwa kipindi kabla ya kwenda njia tofauti.

Mwaka jana, mcheza santuri huyo alizungumza kuhusu jinsi mahusiano yao ya miaka kadhaa yalivyokuwa sumu.

Akiongea kwenye ukurasa wake wa Instagram,  alisema kuwa kazi yake kama DJ ilichangia uhusiano wao mbaya.

“Kama Dj huwa natangamana na wanawake mara kwa mara, shabiki wa kike anaweza kupanda jukwaani na kukupa busu shingoni huku akiomba wimbo na Karen alishindwa kuvumilia. Hata kama hatasababisha drama kwenye hafla hiyo, tunapoingia kwenye gari kurudi nyumbani, ni msomo mpaka nyumbani," alifichua.

DJ Saint aliongeza kuwa walizozana kila siku na kusababisha mvutano ambao ulisababisha kutengana kwao.

"Ilikuwa ni vita baada ya vita, na mimi kuamua kuondoka tulikuwa tumefikia hatua ya kutorudi nyuma. Kila mara ilikuwa mabishano na niliona sio sawa kwa sisi kumlea mtoto wetu katika mazingira hayo. Niliamu kumpa nafasi na ikawa sawa. Ilikuwa ni sumu, kila siku mapigano," Dj Saint aliendelea kusimulia.

Alisema kwamba Karen ni mama mzuri na akabainisha kuwa wanashirikiana vizuri katika malezi ya binti yao.

Akizungumza katika mahojiano na Alibaba kwenye Radio Jambo mwaka wa 2021, baba huyo wa watoto wawili alisema alikutana na Karen kwenye hafla ambayo alikuwa akitumbuiza kama mcheza santuri.

”Nilikutana na Karen kabla ya kuwa mwanasiasa. Alikuwa wakili na nilikuwa kwenye hafla ya DJ,” alisema.

Baada ya kutengana, Karen baadaye alikutana na mwimbaji Samidoh na wakabarikiwa na watoto wawili pamoja.