Kinuthia ajibu swali kuhusu kuwa shoga

Watu wamekuwa wakitilisa shaka jinsia ya tiktoker huyo kutokana na aina ya nguo anazovaa.

Muhtasari

•Shabiki alitaka aeleze wazi iwapo yeye ni shoga, pengine kutokana na mtindo wake wa kuvaa mavazi ya kike.

•Mwanatiktok huyo hakusema ‘ndiyo’ au ‘hapana’ bali alibainisha kuwa swali hilo tayari limepitwa na wakati.

Image: INSTAGRAM// KINUTHIA

Wikendi, mtayarishaji maudhui maarufu nchini Kenya Kelvin Kinuthia alikabiliwa na maswali nyeti kuhusu jinsia na upendeleo wake wa mapenzi.

Shabiki mmoja mwenye udadisi alimwandikia ujumbe kwenye mtandao wa Instagram akitaka aeleze wazi iwapo yeye ni shoga, pengine kutokana na mtindo wake wa kuvaa mavazi ya kike.

"Je, wewe ni shoga," shabiki aliuliza.

Katika majibu yake, mburudishaji huyo hakusema ‘ndiyo’ au ‘hapana’ bali alibainisha kuwa swali hilo tayari limepitwa na wakati.

“Huyu bado anauliza . Heehh, huyu ni kama ako enzi za early man. Hili swali lilipitwa na wakati,” Kinuthia alijibu kwa utani.

Shabiki mwingine alitaka kujua ikiwa yeye ana jinsia mbili au anavaa kama mwanamke ili tu kudumisha chapa yake.

“Sasa intersex ndio nini,” Kinuthia alijibu.

Sio mara ya kwanza kwa Wakenya kuhoji jinsia ya Kinuthia na chaguo lake la mapenzi, watu wamekuwa wakiuliza maswali chungu nzima tangu tiktoker huyo apate umaarufu mwaka wa 2021. Alijizolea umaarufu mkubwa takriban miaka miwili iliyopita wakati tetesi zilipoibuka kuwa alimlaghai mwanamume mwingine baada ya kujifanya mwanamke na baadaye kula nauli ya Ksh344k inayodaiwa kutumwa kwake.

Mwaka jana, mtayarishaji wa maudhui huyo mwenye umri wa miaka 22 aliweka wazi kuwa yeye ni mwanaume.

Wakati wa mahojiano na Mungai Eve, alisema kucheza uhusika wa kike kwenye video zake ni kwa ajili ya burudani na kazi tu.

Kinuthia alibainisha kuwa kamwe hajawahi kukana jinsia yake ya kiume. Hata hivyo aliweka wazi kuwa hayupo tayari kuacha kuigiza kama mwanamke kwa kuwa hiyo ndiyo riziki yake.

"Mimi ni mwanaume. Lakini nilisema siwezi wacha kufanya vitu nafanya kwa sababu watu wameniingililia ati nafanya vile na mimi ni mwanaume. Hiyo ndiyo imenifikisha mahali nipo," Kinuthia alisema.

Alidai kuwa nafasi hiyo ya kike ambayo anacheza imefanya apate kazi za kufanya matangazo ya mavazi na mapambo ya kike.

"Hakuna vile nitaanza kubadilisha mhusika. Hata watu wataboeka. Kuna watu tayari wamezoea jinsi Kinuthia alivyo. Hakuna mahali ambapo nimewahi kusema kuwa mimi sio mwanaume. Ni kazi na hiyo ndiyo imenifikisha mahali nilipo," Alisema.

Katika mahojiano mengine, alidokeza kuwa anapanga kuwa na familia yake katika siku za usoni.

Hata hivyo alibainisha kuwa hatazamii kujitosa kwenye ndoa hivi karibuni  ila baada ya takriban miaka 10.

"Si saa hii, Labda nikiwa na miaka 30 wakati tumemalizana na maisha. Saa hii ni kupiga maisha na kutafuta pesa," Alisema.

Siku za nyuma, mamake Kinuthia aliwahi kusema atafurahia sana wakati ambapo  mwanawe atampelekea binti mkwe.