Mc Jessy adai kutumia mamilioni ya pesa kwa kampeni za 2022

Nilikuwa nashidana na jamaa wa miaka 71 mwanaume ambaye alikuwa amejaribu kuwania kiti hiki kwa mihula minne-Mc Jessy

Muhtasari

• Kuwania kiti cha South Imenti  kulinigarimu zaidi ya shilingi millioni 58.

• Jessy alisema alikuwa na takriban magari 12 kwa msafara wake wa kampeni. 

Mchekeshaji na mwanasiasa Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy
Mchekeshaji na mwanasiasa Jasper Muthomi almaarufu MC Jessy
Image: INSTAGRAM//MC JESSY

Mchekeshaji wa muda mrefu ambaye pia aliwania kiti cha ugombea wa ubunge South Imenti, MC Jessy ,amefichua kuwa kuwania kiti chochote  cha siasa ni gharama mno kwa anayegombea.

Baada ya mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu mchekeshaji huyu alisimulia jinsi ambavyo mambo yalikuwa wakati wa siasa za mwaka wa 2022 licha ya kuwa alipoteza kiti hicho.

"Nilikuwa nashidana na jamaa wa miaka 71 mwanaume ambaye alikuwa amejaribu kuwania kiti hiki kwa mihula minne mbila kufanikiwa kwa kweli kiti hicho kilinigharimu zaidi ya millioni 58,South Imenti  ina maeneo mengi jambo ambalo ilitulazimu tuwe na  gari 12 ...

Kila gari ilizunguka kunipigia debe  kutoka asubuhi hadi jioni bei ya mafuta ilikuwa ghali mno kila gari ilikuwa na mtangazaji ambaye angeuza sera zanguka kwa wenyeji,  wote walikuwa wanataka mshaara wao jioni kwa siku tungetumia zaidi za laki mia tatu". Mc Jessy alisema.

Mc Jessy alisema kwamba kwa siku magari yake pamoja na wasaindizi wake akiwemo meneja wake wa uchanguzi wangetumia zaidi ya elfu 50 kwa kila gari wakati ambapo wangefika maeneo ya kuunza sera zao kwa wakaaji wa maeneo mbunge ya South Imenti.

Mchekeshaji huyu  pia alizungumizia mgombea wa ubunge  Mathare ,Bahati akikiri kuwa  yeye ndiye aliyemtambulisha kwa chama cha UDA ,Bahati alisimulia pia alitumia zaida ya millioni 27 kuwania kiti cha ubunge Mathare licha ya wote kupoteza .