"Maex tuheshimu ndoa" Nduguye Diamond amsuta mwanasoshalaiti kwa kuzungumzia mahusiano yao

Tuerny alikiri kuwa yeye ndiye chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano yake na Jones.

Muhtasari

•Tuerny alidokeza kuwa mahusiano yake na Jones yalikuwa  ni makubaliano tu na hakukuwa na mpango wa kufunga ndoa.

•"Mahusiano ya mwaka 2000 ndio yaongelewe hadi leo jamani!" Jones alisema

Diamond na binamu yake Romy Jones mnamo siku ya harusi yake.
Image: HISANI

Mcheza Santuri mashuhuri wa Bongo,Romy Jones, amemsuta mwanasoshalaiti Tuerny baada ya kuzungumzia mahusiano yao ya zamani.

Tuerny katika mahojiano na Wasafi Media siku ya Jumatatu alithibitisha kuwa alichumbiana na ndugu huyo wa Diamond kwa kipindi kifupi.

Hata hivyo alidokeza kuwa mahusiano yake na Jones yalikuwa  ni makubaliano tu na hakukuwa na mpango wa kufunga ndoa.

"Wakati huo nilikuwa katika miaka fulani ambapo ningeweza kufanya kitu tap tap. Kama ni kudanganya, nilidanganya. Kama ni kuumiza watu niliumiza kwa kipindi hicho. Lakini sio wote ambao nilisema nilikuwa nao ambao ni kweli," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alikiri kwamba ingawa kuna watu kadhaa ambao aliumiza katika kipindi hicho, Romy Jones hakuwa mmoja wao.

Licha ya kutengana kwa muda na hata kuoelewa Ulaya, Tuerny alisema aliporudi Tz alirudiana na Jones na kuendeleza mahusiano.

"Tuligombana na RJ alafu nikaondoka siku hiyo. Niliporudi tulirudiana naye, sidhani kama aliumia kwa sababu ya mtu huyo," alisema.

Tuerny alikiri kuwa yeye mwenyewe ndiye chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano yao ya kipindi kifupi.

"Nilitaka vitu vingi. Nilijikuta nataka mambo mengi. Sikuona nafaa vitu vichache kwa hivyo nikaondoka. Yeye mwenyewe alijua kuwa nafuata vitu vingi," alisema.

Huku akijibu madai ya mwanasoshalaiti huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jones alimkejeli kwa kuzungumzia mahusiano ya zamani.

"Mahusiano ya mwaka 2000 ndio yaongelewe hadi leo jamani!" alisema kwenye Instastori zake.

Jones ambaye kwa sasa yupo kwenye ndoa rasmi pia alimtaka mwanasosholaiti huyo kuipa ndoa yake heshima inayostahili.

"Maex tuheshimu ndoa!" alisema.

Jones alifunga ndoa na mkewe mwezi Disemba 2017 katika harusi ya kifahari iliyohudhuriwa na jamaa wa familia yake na wageni wengine waalikwa.

Mnamo siku ya harusi hiyo, Diamond alimzawadi mcheza santuri huyo nyumba na mamilioni ya pesa.