Morgan Bahati afunguka alivyopoteza nyusi zake baada ya kutumia vipodozi vya Diana Marua

Morgan alibainisha kuwa tukio hilo liliacha athari za muda mrefu kiasi kwamba nyusi zake bado ni fupi hadi sasa.

Muhtasari

•Morgan Bahati amemfichulia Diana alivyopaka bidhaa yake asiyoijua kwenye nyusi zake, bila kutambua madhara ambayo ingemletea.

•Morgan alisema kwamba ingawa alipoteza nyusi zake, hakuhisi maumivu yoyote  wakati wakati wa tukio hilo zima.

Diana Marua na Morgan Bahati.
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mtoto wa kulea wa mwimbaji Kelvin Bahati, Morgan Bahati amefunguka kuhusu tukio la aibu ambalo lililotokea miaka kadhaa iliyopita ambalo lilimwacha bila nyusi.

Wakati akishiriki mazungumzo ya wazi na Diana Marua, mvulana huyo wa miaka 13 alisimulia jinsi takriban miaka mitano iliyopita alipata vishawishi vya kutumia bidhaa za urembo za mamake huyo mlezi baada ya kuachwa peke yake nyumbani.

“Bado nakumbuka mwaka huu, 2018. Ni zamani wakati tulikuwa tunaishi Ruaka. Watu hao walikuwa wamemaliza kukufanyia make up ndani ya nyumba. Kisha ukaondoka kwenda kurekodi video, nilibaki peke yangu nyumbani,” Morgan Bahati alisimulia mama yake.

Aliendelea kumfichulia jinsi alivyopaka bidhaa hiyo asiyoijua kwenye nyusi zake, bila kutambua madhara ambayo ingemletea.

"Nilipokuwa nimekaa, nilipata bidhaa ya kujipodoa kwenye kochi. Sikujua ni nini, nikachukua nikaenda nayo bafu nikapaka kwa nyusi zangu kisha nikajiangalia. Nilipopangusa, nyusi yangu yote ikaenda. Kusoma, nikaona ni gundi ya kope,” alisema.

Mvulana huyo wa miaka 13 alisema kwamba ingawa alipoteza nyusi zake, hakuhisi maumivu yoyote  wakati wakati wa tukio hilo zima.

Alibainisha kuwa tukio hilo liliacha athari za muda mrefu kiasi kwamba nyusi zake bado ni fupi hadi sasa.

“Siku zote nakumbuka tukio hilo. Ni kwa sababu ya tukio hilo kwamba nyusi zangu ni fupi. Watu wana miili tofauti, nywele zangu zinaelekea kukua polepole,” alisema.

Hata hivyo alibainisha kuwa ameona ukuaji wa nyusi zake baada ya kutumia baadhi ya bidhaa za urembo alizotengeneza nyumbani kwao.

"Bado ni fupi, lakini ninashukuru," alisema.

Wakati wa mazungumzo  hayo, mvulana huyo mwenye umri wa miaka 13 pia alifunguka kuhusu jinsi anavyo’miss shule kwani hawezi kutangamana vizuri na marafiki zake wakati huu wa likizo.

Morgan alieleza jinsi anavyoshindwa kuwa na mawasiliano mazuri na ndugu zake kwa vile hawawezi kuelewa mazungumzo anayofanya nao.