"Nimechoka!" Jacque Maribe amuonya vikali Eric Omondi baada ya kudai alikataa DNA kwa mwanawe

"Anadhani uzazi ni uchekeshaji. Anadanganya kuhusu KILA KITU! Acha jina langu na mtoto wangu nje ya vichekesho vyako Eric! Nimechoka,” Maribe alilalamika.

Muhtasari

•Katika taarifa yake , Maribe alitoa onyo kali kwa mchekeshaji huyo na kubainisha kuwa amechoshwa na uwongo wake.

•Maribe alimshutumu mchekeshaji huyo  kwa kuchanganya uzazi na vichekesho na kumuonya dhidi ya kuwaingiza yeye na mwanawe katika uchekeshaji wake.

Eric Omondi na Jacque Maribe

Mwanahabari Jacque Maribe amevunja kimya baada ya mchekeshaji Eric Omondi kumshutumu kwa kuzuia vipimo vya DNA kufanyiwa kwa mvulana wa miaka tisa anayeaminika kuwa ni mtoto wao pamoja.

Katika taarifa kwenye Instastori zake , Maribe alitoa onyo kali kwa mchekeshaji huyo na kubainisha kuwa amechoshwa na uwongo wake.

Mama huyo wa mtoto mmoja alimtaka Eric aseme ukweli na kutishia kutoa ushahidi wa ukweli ikiwa ataendelea kueneza uwongo.

“Nimechoka na hii ujinga. Nimekaa kimya kwa muda mrefu. Huyu muongo anaitwa Eric aseme ukweli au nije na risiti. Na hiyo ni kwisha,” Maribe alisema siku ya Alhamisi.

Maribe alimshutumu mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 41 kwa kuchanganya uzazi na vichekesho na kumuonya dhidi ya kuwaingiza yeye na mwanawe katika uchekeshaji wake.

"Anadhani uzazi ni uchekeshaji. Anadanganya juu ya KILA KITU! Acha jina langu na mtoto wangu nje ya vichekesho vyako Eric! Nimechoka,” Maribe alisema.

Katika  mahojiano na kituo kimoja cha redio cha humu nchini, Eric Omondi alidai kuwa kuna changamoto katika kubaini baba mzazi wa mwanawe Maribe ni nani.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema, "Sasa sijui. Sijui mimi lakini haina shida."

Eric alidokeza kwamba yeye pia husaidia katika kumlea mvulana huyo.

 "Muda mwingine natekeleza lakini muda mwingine pia," alisema.

Alipoulizwa kwa nini hawakufanya kipimo cha DNA ili kusuluhisha kitendawili cha iwapo yeye ndiye baba halisi, alidokeza kuwa kipimo hicho kimekuwa tatizo.

Eric alisema ana hamu ya kufanyika kwa vipimo vya kubaini ni nani baba wa mwanawe Maribe, “Kuna venye nimekuwa nikitaka.” aliendelea.

Mtangazaji alipomtaka athibitishe kama Maribe ndiye tatizo, Eric alisema, “Baaas ..sitaki kuongelea sujui kuna laywer nini, lakini napoenda venye wewe umeishika. Kuna orders sitaki kuongelea sasa nimefurahi venye umesema wewe."

Mwaka wa 2021,  mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 41 aliibua madai kuwa anashuku mtoto wa Maribe sio wake. Alidai kwamba aliwahi kumshinikiza mwanahabari huyo wafanye vipimo vya DNA ili kuthibitishahilo  ila akakataa.

Wakati huo, Maribe kwa upande wake alidai kwamba mzazi huyo mwenzake hakuwa anasaidia katika malezi ya mtoto wao.