Hongera! Orodha ya Wakenya mashuhuri waliohitimu kutoka vyuo vikuu mwaka wa 2023

Idadi kubwa ya watu mashuhuri wa Kenya wametunukiwa shahada mbalimbali mwaka huu.

Muhtasari

•Babushka  alifichua kwamba alitunukiwa shahada ya sheria baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kisii.

•Akothee alihitimu Desemba na kupata shahada ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Mt Kenya

ni miongoni mwa Wakenya mashuhuri waliohitimu 2023.
Akothee, Babushka na Waihiga Mwaura ni miongoni mwa Wakenya mashuhuri waliohitimu 2023.
Image: HISANI

Mtayarishaji maudhui mashuhuri wa Kenya Kennedy Rioba almaarufu Babushka Kenya  mnamo siku ya Jumanne alishiriki habari za kusisimua kuhusu kuhitimu kwake kutoka Chuo Kikuu.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, mtayarishaji huyo wa maudhui mwenye ulemavu wa miguu alifichua kwamba alitunukiwa shahada ya sheria baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kisii.

Mshauri huyo alibainisha kuwa safari ya masomo haikuwa rahisi lakini akamshukuru Mungu na watu wengine ambao wamemsaidia na kumsapoti..

"Safari imekuwa ndefu na ya kuchosha, iliyojaa dhoruba lakini MUNGU amefanya kwa niaba yangu. Imekuwa MUNGU na itabaki kuwa Mungu Daima���❤️,” Babushka alisema.

Aliongeza, "Nimefurahishwa sana na sura inayofuata ya Maisha Yangu❤️���.Asante  Oga Obinna Kwa Zawadi��� na Shukrani zangu kwenu nyote kwa Usaidizi na Upendo Wenu Usio na Mwisho kuelekea Mafanikio haya katika maisha na Kazi yangu yote . Mungu awabariki ninyi nyote. HONGERA SANA KWANGU.”

Mamia ya Wakenya wamejitokeza kumpongeza mtayarishaji maudhui huyo  kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikan siku ya Jumanne.

Babushka hata hivyo sio mtu mashuhuri wa Kenya pekee ambaye amehitimu mwaka huu, mastaa wengine kadhaa mashuhuri wametunukiwa digrii tofauti mnamo 2023.

Hii hapa orodha ya watu wengine mashuhuri ambao wamehitimu mwaka wa 2023;

1. Kennedy Rioba almaarufu Babushka Kenya (Muundaji Maudhui) - Alihitimu Desemba na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Kisii.

2. Esther Akoth almaarufu Akothee (Mwanamuziki na mjasiriamali) - Alihitimu Desemba na kupata shahada ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Mt Kenya.

3. Flora Limukii (Mwanahabari) - Alihitimu Desemba na shahada ya Uandishi wa Habari wa Matangazo kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

4. Waihiga Mwaura (Mwandishi wa Habari) - Alihitimu Novemba na Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano (Masomoy ya Uandishi habari) kutoka Chuo Kikuu cha Daystar.

5. Dr Mercy Korir (Mwanahabari) - Alihitimu Oktoba na Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara katika Masoko na Fedha.

6. Fancy Makadia (binti ya Akothee) - Alihitimu Februari kutoka chuo kikuu cha Paris, Ufaransa.