"Inahuzunisha!" Akothee achukizwa na kijana aliyekiri anafurahia kushiriki mapenzi na mtoto

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alilaani kitendo hicho kiovu na akataka kukamatwa kwa mtu huyo.

Muhtasari

•Akothee alichapisha screenshot ya chapisho la Facebook ambapo mtumiaji kwa jina Smata Sam alionyesha picha ya kijana na ya msichana mdogo ambaye alidai ni mshirika wake wa mapenzi.

•"Hii inasikitisha na kuudhi, popote alipo, mtu huyu anapaswa kukamatwa. Kama ni jirani yako tuambie tumuendee,” Akothee alisema.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amemkashifu mtumizi mmoja wa mtandao wa Facebook ambaye alijigamba kuhusu kufanya mapenzi na msichana mdogo bila majuto.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Akothee alichapisha screenshot ya chapisho la Facebook ambapo mtumiaji kwa jina Smata Sam alionyesha picha ya kijana na ya msichana mdogo ambaye alidai ni mshirika wake wa mapenzi.

Katika sehemu ya maelezo, mtumiaji huyo wa Facebook alidai kuwa haogopi kulala na msichana huyo mdogo kwani hawezi kukamatwa.

“Mungu wangu nimeliona hili na siwezi kunyamaza. Wazazi, jihadharini na nani mnamwacha mtoto wenu. Mayoooo, huyu ni mbakaji au mnajisi wa watoto?” Akothee alisema kuhusu chapisho hilo.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alilaani kitendo hicho kiovu na akataka kukamatwa kwa mtu huyo.

"Hii inasikitisha na kuudhi, popote alipo, mtu huyu anapaswa kukamatwa. Kama ni jirani yako tuambie tumuendee,” alisema.

Katika screenshot zilizochapishwa na mama huyo wa watoto watano, mtumiaji huyo wa Facebook alijigamba kwamba anapendelea kujihusisha kimapenzi na msichana huyo mdogo kuliko wanawake wazee.

Chapisho hilo lilivutia ukosoaji zaidi kutoka kwa wanamitandao wengine huku wengi wakionekana kulaani kitendo cha mtumiaji huyo wa Facebook na kutaka aadhibiwe.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao;

Tspark_k:  I think the guy should not be arrested, he needs to have a little conversation with the mob kidogo tu then the police take him. This is disgusting.

Detty_richard: He should be castrated!!!

Cosmayahansen: Yesu wangu.. eeh huyu ni shetani mkubwa, uwii akapimwe akili kwanza.

Mulhat_muhando: Hii serikali badala ya kuleta sheria hazisaidii, they should pass a law that claims rapists and pedophiles should be killed once found guilty. Mimi sijawahi eti ooh he is someone’s son!!  Akifanya hakuona anaumiza mtoto wa mtu.

_dennohgram: Ama upate ni setup, juu mi sioni niaje pedophile anaweza jipost akisema ye hukula mtoi, probably someone’s behind it.