Mashabiki wa Rhumba kumkaribisha Koffi Olomide Kenya Desemba, lakini je, Koffi ni nani?

Jambo ambalo huenda hujui ni kwamba katika ujana wake alitakiwa kuwa mwanasoka wa kulipwa lakini baadaye alijikita kwenye muziki.

Muhtasari

•Jiunge na Radio Africa katika kumkaribisha Koffi tena katika jiji letu  kwa tamasha la kufana mnamo tarehe 8, 9, na 10 Desemba

Koffi Olomide
Koffi Olomide
Image: Facebook

Antoine Christophe Agbepa Mumba, almarufu Koffi Olamide ni mwimbaji wa soukous nchini Congo, mtayarishaji, mtunzi wa nyimbo, , kiongozi wa bendi, na mwanzilishi wa Quartier Latin International.

Alizaliwa mwaka 1956, Julai 13 Kisangani, Ubelgiji DRC, na alikulia katika wilaya ya Lemba ya Kinshasa hadi familia yake ilipohamia Lingwala mnamo 1973.

Jambo ambalo huenda hujui ni kwamba katika ujana wake alitakiwa kuwa mwanasoka wa kulipwa lakini baadaye alijikita kwenye muziki baada ya kuhamasishwa na rumba ya Congo ya shule ya zamani.

Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo mbalimbali  alianza kupiga gitaa la nyuzi sita chini ya mshauri Papa Wemba.

Anajulikana kwa ujuzi wake wa kusokota  kiuno,  alipata umaarufu wake katika mwaka wa 1977 baada ya kuachilia kibao  'Princesse ya Synza' ambayo aliwashirikisha Papa Wemba na King Kester,

Wimbo ambao imfanya kuwa Mwimbaji-Mwandishi wa Nyimbo bora zaidi nchini Zaire.

Wimbo huu ulimpatia umaarufu ambapo baadaye mwaka wa 1986 aliongoza na kuanzisha Quartier Latin International ambapo alianza kutoa albamu zake baadaye mwaka wa 1992.

Aliwashirikisha wasanii wengi kama Fally Ipupa, Jipson Butukondolo, Deo Brondo, na wengine wengi.

Kulikuwa na tetesi mwaka 1987 kuwa aliugua UKIMWI akiwa Ulaya jambo ambalo liliathiri sana kazi yake (zama hizo ilikuwa ni suala zito) na kumfanya ajibu kwa mtindo wa wimbo, ‘Ngulupa’ hujaona chochote, umesikia tu usiongee usiyoyajua; kuhara kwa maneno ni jambo baya,"wimbo ulisema.

Amekuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miongo kadhaa akiwa na tajriba ya takriban miaka 40 na ndiye Mwafrika wa kwanza kabisa kuonyeshwa katika Palais Omnisports de Paris-Bercy na mmoja wa wanamuziki 12 wa Kiafrika walioorodheshwa katika Albamu 1001.

Koffi olomide
Koffi olomide

Mnamo Desemba 4, 2005, alishinda toleo la 10 la Tuzo za KORA, akipokea Tuzo ya Mafanikio ya Maisha nchini Afrika Kusini ambayo ilikuja na zawadi millioni kumi na tano.

Koffi Olomide ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa muziki wa Congo na Afrika.

Jiunge na Radio Africa katika kumkaribisha Koffi tena katika jiji letu  kwa tamasha la kufana mnamo tarehe 8, 9, na 10 Desemba

Tikiti zinapatikana kwenye link zifuatazo;

 https://ticketyetu.com/r/oDs

 https://ticketyetu.com/r/IQJ