Radiojambo kuadhimisha siku ya Reggae K1 Klub House Parklands Alhamisi

Muhtasari
  • Radiojambo kuadhimisha siku ya Reggae K1 Klub House Parklands Alhamisi

Huku mashabiki wa nyimbo za Reggae wakipanga kuadhimisha World Reggae day siku ya Alhamisi tarehe 1 Julai, kituo cha Radiojambo kimehakikisha kwamba kitawatumbuiza mashabiki wake vilivyo.

Njoo kwenye K1 Klub House pale Parklands upatane na watangazaji wako uwapendeo kuanzia saa nane mchana hadi saa moja usiku.

Baadhi ya watangazaji ambao watakuwa katika eneo hilo ni pamoja na Lion, Mbusi,Ghost MUlee miongoni mwa watanzaji wengine.

Siku ya Kimataifa ya Reggae ni tukio la kila mwaka lililofanyika Kingston, Jamaica, na imejitolea kusherehekea mtindo huu wa muziki ambao uliingia ulimwenguni katika nchi ya kisiwa kidogo katika Caribbean.

Ilichukua muda, lakini reggae hatimaye ililipuka kugusa kila kona ya dunia na mtindo wake usio wa kawaida na wenye kuvutia,

Reggae ikawa mtindo wa nguvu wa muziki na mizizi ya kina wakati Bob Marley alijiunga na muziki huo na ushawishi wake haujawahi kusimamishwa kukua katika zaidi ya karne nyingi.

Mbogi ya reggae mpooo! Fomu imejipa pale K1 Klub House Parklands kesho kuanzia saa nane tunaposherehekea #WorldReggaeDay. Njoo uhangout na akina Lion Deh , Gravitti, Ghost Mulee na wengine! #Jambo1Love

Posted by Radio Jambo on Wednesday, June 30, 2021

Mtindo wa reggae umefanya alama yake na kuenea pana, na tani za mitindo tofauti na tofauti zinazoendelea.

Haya basi siku ya Alhamisi njoo ujivinjari na watangazaji wako wa radiojambo, lakini jambo la muhimu mashabiki wote wataohudhuria hafla hiyo wanaulizwa kufuata kanuni za wizara ya afya ili kuthibiti kusambaa kwa maambukizi ya corona.