'Ninakupenda wewe ulivyo sasa,'Ujumbe wake Wahu kwa mumewe Nameless

Muhtasari
  • Wahu asherehekea siku ya kuzaliwa na Nameless
  • Haya yanajiri siku moja baada ya kitinda mimba wao kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pia
  • Wahu alimshukuru Nameless kwa kuwa baba wa watoto wake na mume wake huku akiri kwamba anampenda jinsi alivyo
Nameless na Wahu
Nameless na Wahu
Image: Hisani

Msanii Wahu na Nameless wamekuwa katika ndoa kwa zaidi ya miaka 15, huku Nameless akisherehekea siku yake ya kuzaliwa Wahu alimwandikia ujumbe wa kipekee.

Haya yanajiri siku moja baada ya kitinda mimba wao kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pia.

Wahu alimshukuru Nameless kwa kuwa baba wa watoto wake na mume wake huku akiri kwamba anampenda jinsi alivyo

Hivi karibuni tumeaona wanandoa hao wakita bidii kwenye usanii wao.

Huu hapa ujumbe wake Wahu kwa Nameless;

"Alililililiiiii !!!!! Nadhani ni siku ya kuzaliwa ya nani leo !!!!!!!! πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸŽ‰πŸ˜πŸ’– Heri ya kuzaliwa kwa Mkuu wangu wa Nyumba !!! @namelesskenya Kuangalia siku zako za kuzaliwa 20+ ambazo tumesherehekea, nimeona umekua kwa njia zaidi ya moja.

Ninakupenda wewe uliye sasa, na siwezi kusubiri kuona kilicho mbele ya safari ya maisha yako!

Wewe ni mwanamume wa kushangaza na wala sio kamili.. (uto tu moods twako saa zingine πŸ™„πŸ™„πŸ€¦πŸΏβ€β™€οΈπŸ˜…) lakini ni nani kamili .... Fam, tafadhali ungana nami kumtakia heri njema ya kuzaliwa mshauri kwa wengi, baba wa watoto wangu na mpenzi  wa maisha yangu ... siku ya kuzaliwa yenye furaha na heri sana leo. Nakupenda babe πŸ’˜πŸ’˜," Wahu Aliandika.