Mtakufa bila watoto! Kibe awasuta wanawake wasiotaka kubeba mimba

Muhtasari

• Aliyekuwa mtangazaji wa redio, Andrew Kibe ametoa maneno makali kwa wanawake wote wasiotaka kupata watoto.

• Kupitia kwa video aliyoiachia katika mtandao wake wa Instagram, Kibe amesema kwamba hakuna kitu cha kuridhisha nafsi ya mwanamke kama kutumia tumbo lake la uzazi vizuri kubeba watoto na hatimaye kujifungua.

Andrew KIbe
Andrew KIbe
Image: Instagram KWA HISANI

Aliyekuwa mtangazaji wa redio, Andrew Kibe ametoa maneno makali kwa wanawake wote wasiotaka kupata watoto.

Kupitia kwa video aliyoiachia katika mtandao wake wa Instagram, Kibe amesema kwamba hakuna kitu cha kuridhisha nafsi ya mwanamke kama kutumia tumbo lake la uzazi vizuri kubeba watoto na hatimaye kujifungua.

Kibe ameonya kuwa iwapo hawatafanya maamuzi ya kibusara sasa, watawaumbua daktari wakitimu miaka arobaini na mitano kutafuta jinsi wanaweza kupata angalau hata motto mmoja.

Kulingana na Kibe, afadhali uzeeke na kungóka meno ukiwa tayari una watoto kuliko kuzeeka bila kufanikiwa na motto hata mmoja.

Kauli hii inajiri siku chache tu baada ya msanii kutoka Marekani, Rihanna kuweka wazi mimba yake kwa umma huku akiwa amepiga picha na mpenzi wake. Kibe ameoneza kuwa kuna wasanii wengi wa kike tena wenye hela nyingi ambao wamekubali kubeba mimba ila kuna wale hasa kutoka Kenya ambao wamedinda kabisa kwa sababu ambazo mtangazaji huyo anasema hazina maana na zimepitwa na wakati.

Idadi kubwa ya mashabiki hasahasa wanaume wameonekana kufurahishwa na kauli hiyo huku kina dada wakimjia juu na kumtaka ashughulike na maisha yake.