Adhiambo yafikisha views 10m, Bahati awashukuru mashabiki

Muhtasari

• Msanii Kevin Bahati amewashukuru mashabiki wake kwa kuwezesha wimbo wake aliomshirikisha Prince Indah kufikisha views milioni kumi.

• Ifahamike kwamba ni miezi mitatu sasa tangu wimbo huo upakuliwe katika mtandao wa YouTube huku ukionekana kuwateka mashabiki wengi ambao walionekana kupenda wimbo huo kwa dhati.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Msanii Kevin Bahati amewashukuru mashabiki wake kwa kuwezesha wimbo wake aliomshirikisha Prince Indah kufikisha views milioni kumi.

Akiwa amepakia video ya ngoma hiyo katika mtandao wake wa Instagram, Bahati ameonyesha furaha yake kwa hatua hiyo akisema kwamba wimbo huo umeweka rekodi mpya.

“Wimbo wa Adhiambo umefikisha views milioni kumi. Huu ni ushindi mwingine. Hii ni rekodi nyingine,” aliandika Bahati.

Ifahamike kwamba ni miezi mitatu sasa tangu wimbo huo upakuliwe katika mtandao wa YouTube huku ukionekana kuwateka mashabiki wengi ambao walionekana kupenda wimbo huo kwa dhati.

Aidha Bahati alisema kwamba akimaliza kumzawidi mkewe katika siku ya valentino basi ataingia studioni kuandaa kazi nyingine kwa mashabiki wake, ikiwa kwamba hajatoa wimbo wowote katika siku za hivi karibuni.

Swali ambalo wengi wa mashabiki na pia washikadau wa burudani wanazidi kujiuliza ni iwapo Bahati atatoa ngoma ya kibinafsi au atamshirikisha msanii mwengine katika kolabo.