Ringtone Apoko ajigamba kuhusu kupatia binti ya Bahati zawadi zenye gharama ya 100,000

Muhtasari

•Heaven ambaye ni mtoto wa kwanza wa Bahati na bibiye Diana Marua alihitimu miaka minne wiki iliyopita.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Wikendi iliyotamatika karamu ya kufana iliandaliwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye Bahati , Heaven Bahati.

Heaven ambaye ni mtoto wa kwanza wa Bahati na bibiye Diana Marua alihitimu miaka minne wiki iliyopita.

Watu kadhaa ikiwemo wanamuziki na watu mashuhuri walihudhuria karamu ya kusherehekea siku hiyo maalum kwa familia ya Bahati.

Mmoja wa wasanii waliokuwa wamealikwa ni Ringtone Apoko ambaye alitumbuiza kwa nyimbo kadhaa na kuburudisha wageni.

Baada ya sherehe, Apoko alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kujigamba kuhusu kumpatia bintiye Bahati zawadi zenye thamani ya shilingi laki moja.

Apoko ambaye hujitambulisha kama mwenyekiti wa muungano wa wanamuziki wa injili aliendelea kudai kuwa zawadi zaidi kutoka kwake zitamfikia Heaven hivi karibuni.

Nilihudhuria sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mtoto wa Bahati na nikampa zawadi za jumla ya Sh100k. Zaidi zinakuja, heshimu mwenyekiti" Ringtone alandika chini ya picha iliyoonyesha akiwa na Bahati pamoja na Heaven.

Ringtone hata hivyo anajulikana kujigamba kuhusu utajiri wake mkubwa na mambo makubwa yanayomgharimu  pesa nyingi.

Mara nyingi Ringtone ameshtumiwa kutumia hafla kama ile kutafuta kiki.