Vanessa Mdee adai hakuwa na mpango wa kuwa mama

Muhtasari

•Msanii wa kike Vanessa Mdee amefunguka kuhusu  mahusiano yake na mume wake, Rotimi huku akibaini ndiye alifanya habadilishe msimamo wake na kuwa mama

Vanessa Mdee
Image: Hisani

Msanii wa kike Vanessa Mdee amefunguka kuhusu  mahusiano yake na mume wake, Rotimi huku akibaini ndiye alifanya abadilishe msimamo wake na kuwa mama.

Wawili  hao ambao wamefungua app ya  burudani  wamekuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja.

Kulingana na Vanessa, mambo ya kuwa mzazi hayakuwa kuwa kwenye akili yake kitambo lakini aliomba watu wasije wakatafsiri kauli hiyo vibaya.

"Mnafaa kuelewa, kwa sababu kama mlikuwa mnanijua  kitambo sikuwahi  kuwa na mipango ya kuwa mama, hata sikuwa nafikiria kuwa mama  ila mtazamo wangu ulibadilika wakati nilikutana na mpenzi wangu Rotimi ambaye alifanya nibadilishe mawazi yangu na kumzalia  mtoto mmoja basi nikakubali, lakini msinielewe vibaya kuwa napenda watoto," alisema Vanessa.  

Vanessa ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafurahia maisha ya kuwa kwenye ndoa. Ni  mwaka jana ambapo alieleza kuacha kuimba kwa muda huku akieleza masaibu ya wanamuziki.