Soma mambo ambayo huku yafahamu kuhusu msanii Alikiba

Muhtasari
  • Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu  kwenye ndoa
Image: INSTAGRAM// ALI KIBA

Mkewe Mwanamuziki nguli wa Tanzania Alikiba, Amina Khalef amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka kutengana mume wake.

Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu  kwenye ndoa.

Alieleza kuwa  sababu kuu ya kuvunja ndoa yake na mwanamuziki huyo ni kuwa na msongo wa mawazo na kutelekezwa na mumewe huku akibaini  kuwa Ali Kiba hatekelezi majukumu kama mume.

Alikiba amevuma baada ya uvumi huo, licha ya hayo amekuwa msanii anayetambulika kwenye tasnia ya muziki.

Haya haapa baadhi ya mambo ambayo huku yajua au kuyafahamu kuhusu msanii huyo;

  1. Nyota huyo  sasa ana umri wa miaka 36
  2. Ndiye mwanzilishi wa Kings Music Records
  3. Ali Kiba ni rafiki wa karibu wa Gavana Joho ambaye pia anapata talaka kutoka kwa mke wake wa Italia
  4. Kiba ni baba wa watoto watano wawili na mke wake Mkenya Amina Khalef
  5. Jina lake halisi ni Ali Saleh Kiba
  6. Anatoka Kigoma, Tanzania
  7. Kiba alifunga ndoa na Amina Khalef mnamo 2018, wawili hao walikuwa wamefahamiana tangu 2016