Natamani ugomvi wa kuvunjika kwa ndoa yangu ungeisha haraka - KRG

Joho amekubali kutoa talaka kwa mkewe baada ya agizo la mahakama

Muhtasari

• KRG ameshabikia jinsi gavana Joho ameshughulikia suala la kutoa talaka kwa mkewe kwa haraka mno jinsi alivyotakiwa na mahakama

• Msanii huyo anasema pia anasikitika kwa nini yake ilichukua muda kumalizika rasmi baada ya kutofautiana na mkewe

Rappa KRG the Don
Image: INSTAGRAM/KRG

Msanii wa dancehall, KRG the Don amefurahia kwamba ugomvi wa kuvunjika kwa ndoa ya gavana wa Mombasa Hassan Joho umeisha haraka na kusikitika kwamba anatamani hata ugomvi wa ndoa yake kuvunjika ungeisha haraka hivyo.

KRG ambaye ndoa yake na mkewe Linah Wanjiru mwishoni mwa mwaka 2021 kwa kile alisema kwamba mkewe alikuwa mzembe mpaka akaanza kuzurura na machokoraa, anasema mgogoro wa kuvunjika kwa ndoa yake ulichukua muda sana mahakamani na mpaka kutoa talaka alikuwa amezungushwa mno

Anasema mgogoro wa kuvunjika kwa ndoa ya Joho umekamilika haraka na ameshabikia gavana huyo kwa kufanya hima kwani jambo hilo linafyonza sana linapochukua muda.

“Gavana Joho amekubali kutoa talaka kwa mkewe Muitaliano Giovanni Fazzini, ninatamani yangu pia ingekamilika kwa haraka namna hii,” aliandika KRG kwenye instastories zake.

Image: INSTAGRAM

Ndoa ya gavana Joho ilipata msukosuko mkubwa hivi majuzi wakati mkewe huyo wa takribani mwongo mmoja kuelekea katika mahakama ya Kadhi jijini Mombasa na kudai talaka yake kwa kile alichokitaja kuwa gavana Joho amekuwa akimtelekeza tangu mwaka 2013.

Mahakama ilimpa Joho muda wa siku saba kujibu madai hayo na gavana Joho hatimaye amekubali kutimiza ombi la mkewe huyo kwa kutoa talak ana hivyo ndoa hiyo kufikia kikomo.