Alikiba ashindwa kutekeleza majumu ya kiume, Mke ataka talaka

Muhtasari

• Amina Khalef amewasilisha kesi mahakamani kutaka kutengana na Alikiba.

• Alikiba amejiunga na watu mashahuri ambao wanatarajiwa kutalikiana na wake zao mwaka huu.

Ali Kiba na mkewe Amina
Ali Kiba na mkewe Amina
Image: hisani

Mkewe Mwanamuziki nguli wa Tanzania Alikiba, Amina Khalef amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka kutengana mume wake.

Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu  kwenye ndoa.

Alieleza kuwa  sababu kuu ya kuvunja ndoa yake na mwanamuziki huyo ni kuwa na msongo wa mawazo na kutelekezwa na mumewe huku akibaini  kuwa Ali Kiba hatekelezi majukumu kama mume.

Wawili hao walioana mwaka wa 2018, chini ya kanuni za Kiislamu ambapo waliandaa sherehe kubwa mjini Mombasa huku mashabiki wakitaja harusi hiyo kuwa ya kupigiwa mfano.

Ali Kiba amejiunga na watu mashahuri ambao wanatarajiwa kutalikiana na wake zao mwaka huu.

Isitoshe rafiki wa Alikiba, gavana Hassan Joho pia amekubali na kutia saini  ombi la mkewe ambaye alikuwa amewasilisha talaka mahakamani.