Nyashinski afuta picha zote Instagram, anafollow mkewe pekee

Muhtasari

• Nyashinski amefuta picha na video zote kwenye instagram yake na kumfollow mkewe pekee

Nyashinski
Nyashinski
Image: Hisani

Mwanamuziki tajika wa mitindo ya kufokafoka nchini Kenya Nyashinski amewaacha wengi wakishangaa nini kinaendelea katika Maisha yake baada ya kufuta picha na video zote kwenye ukurasa wake wa Instagram

Mwanamuziki huyo ana utata sana haswa kwa vitendo vyake mitandaoni, kwani akaunti yake ya Instagram ina wafuasi wanaomfuata Zaidi ya laki sita huku yeye akiwa anamfuatilia mkewe pekee na kupuuza hata marafiki wake wa karibu.

Wikendi iliyopita akipiga bonge la show katika ukumbi wa maduka ya jumla, Two Rivers jijini Nairobi, Nyashinski aliwaahidi wafuasi wake kwamba ana mipango ya kuwajengea jiji ambalo alidokeza litakwenda kwa jina la Nyashinski.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo anamfuata Zia Bett ambaye ni mke wake pekee na hapendi sana vitimbi  vya kutafuta kiki mitandaoni.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana, Nyashinski alimsomea mtu ambaye alikuwa anatumia jina lake kwenye mtandao wa Twitter na kuwalaghai watu fedha.

Maoni yako ni yepikuhusu ufuasi wa mitandaoni. Je, ni vizuri mtu kurudisha ile inaitwa kwa kimombo follow back kwa wafuasi na Rafiki wa karibu wanaomfuata mitandaoni?