'Fanya unachokipenda' Nyashinski awashauri mashabiki wake

Muhtasari

• Mwanamuziki Nyashinski amewashauri mashabiki wake kujituma zaidi kwa kazi wanazozifanya bila kujali  changamoto wanazozipitia.

Nyashinski
Nyashinski
Image: Hisani

Mwanamuziki Nyashinski amewashauri mashabiki wake kujituma zaidi kwa kazi wanazozifanya bila kujali  changamoto wanazozipitia.

Akizungumza wakati wa hafla ya Love, Wine na Vibes ambayo ilikuwa imeandaliwa eneo la Two Rivers, alichukua muda mfupi jukwaani kuwapa ushauri  mashabiki  hao, huku hakiwaonya dhidi ya kutokata  tamaa kwa jambo lolote wanalopanga kutekeleza maishani.

“Unaeza kuchukua tahadhari, unaweza kuwa mtu mwenye manufaa, sio lazima uwe umetoka kwenye familia tajiri, sio lazima utoke kwenye familia maskini, lakini unaweza kuwa mtu unamtamani maishani,”

Rapa huyo ambaye amekuwa kwenye ulingo wa muziki kwa muda mrefu alikiri kwamba  umri wake unazidi kuongezeka na hivyo ana mipango kabambe  ya kujenga jiji lake ( Nyashinski City)  kwa ajili ya mashabiki wake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipenda kazi zake.

Vilevile, aliwashauri wasanii kufanya kitu ambacho wanakipenda na kufuata ndoto zao bila kujali changamoto wanazokumbana nazo.

“Kwa wasanii wote, fanya kile unachopenda. Kazi yangu na maisha yatawafundisha watu kuwa wanaweza kuwa kile wanakitamani maishani, wanaweza kuota, wanaweza kuwa kitu. Sio lazima kutoka kwa familia tajiri au maskini,” alisema.