Jitahidi usimuumize mtu yeyote-Fridah Kajala kwa mashabiki

Muhtasari
  • Kajala alivuma sana mwaka jana baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa bongo Harmonize
Muigizaji Fridah Kajala
Image: Fridah Kjala/INSTAGRAM

Kama umekuwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii, jina la Fridah Kajala unapoliona kwa hakika sio geni kwako.

Kajala alivuma sana mwaka jana baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa bongo Harmonize.

Alizidi kuvuma baada ya wawili hao kuachana, kwani uhusiano wao haukudumu sana.

Kwa muda sasa Kajala amekuwa akishiriki neno la kuwatia moyo mashabiki wake, na hata kuwapa ushauri kwa jambo moja au lingine.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama siku ya Ijumaa, muigizaji huyo maarufu aliwahimiza mashabiki wake wawe makini kutomuumiza mtu yeyote kwani kuna baadhi ya watu ambao hawana watu wa kuwafariji.

"JItahindi usimuumize mtu yeyote,Watu wengine hawana watu wa kuwafariji," Aliandika Kajala.

Kupitia kwenye chapisho lingine alisema kuwa;

"Unapaswa kuhisi kupendwa bila, kuhisi kwamba unaomba kupendwa."