TID asuta 'media' ambazo zilidinda kucheza muziki wake

Muhtasari

• Msanii kutoka Tanzania, TID amesema kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilidinda kucheza ngoma zake kwa lengo la kuzima kipaji chake.

• Amewataka washikadau wote wa burudani nchini humo kuhakikisha kwamba wanajenga mazingira faafu kwa kila mtu mwenye kipaji kutasua na kutimiza ndoto zake za maisha.

tid1
tid1

Msanii kutoka Tanzania, TID amesema kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilidinda kucheza ngoma zake kwa lengo la kuzima kipaji chake.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Salama Jabir, TID alisema kwamba licha ya changamoto hizo ameendelea kufanya vizuri katika muziki na kwamba maisha yake yameendelea vizuri.

Vilevile aliendelea kusema kwamba hulka yake ya kukosoa vituo vingi vya habari kuhusu namna ya kuendesha mambo yao, ilimchonganisha na watu wengi , jambo ambalo lilimpelekea kupoteza hela nyingi ambazo angezipata kupitia muziki wake.

Mwanamuziki huyo amesema kwamba licha ya kukosa kupanda jukwaani kwa muda mrefu, alifanikiwa kutafuta mbinu na biashara mbadala za kuleta chakula kwenye mezani, jambo ambalo anaamini linazidi kumfanya awe kidedea kwenye gemu la Bongo.

TID pia ameweka wazi kwamba kuna asilimia kubwa ya wasanii ambao amewashika mkono na hata kuwakutanisha na wasanii wengine wakubwa ili washirikiane kwenye kazi mbalimbali za kimuziki ila ukwasi wake bado haujatambulika ipasavyo.

Amewataka washikadau wote wa burudani nchini humo kuhakikisha kwamba wanajenga mazingira faafu kwa kila mtu mwenye kipaji kutasua na kutimiza ndoto zake za maisha.

Ifahamike kwamba amefahamika sana pia kupitia ukwasi wake katika mazungumzo na misimamo yake kuhusu mambo mbalimbali yanayotendeka katika muziki na jamii kwa ujumla.