Aliyekuwa muigizaji wa Kanumba apata ajali ya barabarani

Muhtasari

• Emmanuel Myamba aliyekuwa akiigiza kama mchungaji na ambaye kwa sasa ni mhubiri anasimulia alipata ajali mbaya ya barabarani pamoja na familia yake.

Ajali ya gari la Pastor Myumba
Ajali ya gari la Pastor Myumba
Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa muigizaji mwenza katika filamu nyingi za marehemu Steven Kanumba, Emmanuel Myamba amedhibitisha kupata ajali mbaya sana wikendi iliyopita ila wakapona bila majeraha mabaya.

Myamba ambaye wengi wanamfahamu kwa kuigiza kama mchungaji au mhubiri katika filamu za Kanumba kwa sasa ni mhubiri wa kanisa la House of Victory nchini Tanzania.

Emmauel Myamba ama Pastor Myamba kama anavyojiita katika huduma ya injili ameandika kwenye Instagram yake na kusimulia kwamba jana walipokuwa wakiondoka kwenye mlima wa maombi kuelekea kanisani pamoja na familia yake, gari lao lilipata ajali mbaya sana ila akasema wako imara bila maumivu makali.

Tunamshukuru sana Mungu atulindaye na kutupa uzima siku zote, siku ya jana tukiwa tunatoka Mlima wa maombi kuelekea kwenye ibada, mimi pamoja na familia yangu, tulipata ajali hiyo mbaya…Kwa jinsi Mungu alivyomwema sana kwetu, alituokoa sote na mauti na wote tu wazima sana hakuna hata aliyechubuka kwa jereha lolote. Tunamtukuza Mungu sana sana. Ungana nami, kumshukuru Mungu kwa ajili yangu na familia yangu.” Aliandika Myamba kwenye Instagram yake akiambatanisha picha ya gari hilo lilivyokuwa limebingiria.