Mamake Kanumba amsamehe muigizaji Lulu kwa mauaji ya mwanawe

Muhtasari

• Lulu alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kumuua bila kukusudia muigizaji huyo mashuhuri Kanumba mnamo mwaka wa 2017.

Muigizaji Lulu
Muigizaji Lulu
Image: Hisani

Muigizaji  wa Filamu za Bongo Frida Mtegoa amefunguka na kueleza kuwa alimsamehe Muigizaji Elizabeth Michael almaarufu Lulu aliyesababisha kifo cha mwanawe Stephen Kanumba.

Lulu alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kumuua bila kukusudia muigizaji huyo mashuhuri Kanumba mnamo mwaka wa 2017.

Frida mtegoa, mama wa Kanumba alieleza kilichomfanya yeye kujitosa kwenye uigizaji ni kutokana na kifo cha mwanawe kwa sababu hakuwa na kazi ya kufanya ili kupata pesa za kujimudu.

 Mama wa Kanumba alieleza kuwa alitamani sana kuona Lulu akimletea mjukuu ila akaeleza yaliyotokea yamepita na ameyasahau. 

Akihojiwa na runinga ya Global,Mama Kanumba alisema amesahau yote yaliyotokea na kueleza kuwa matamanio yake yalikuwa kuigiza na Lulu ili kuonyesha upendo wake kwake.

 

"Popote alipo ajue kwamba sina chochote kibaya dhidi yake, laiti wangenipa mjukuu wakati huo walikuwa wakichumbiana,"alisema Mama Kanumba.

 

 

Elizabeth alituhumiwa kumsukuma Kanumba kwa nguvu, ambapo alianguka na kupata pigo baya kichwani, jeraha ambalo lilisababisha kifo chake.

Lulu aliachiliwa kutoka gerezani na kuruhusiwa kutumikia kifungo cha nyumbani mwaka wa 2018.