Weezdom afunguka 'beef' yake na Bahati ilivyoanza

Muhtasari

• Weezdom amefunguka kwamba tofauti zao na Bahati zilitokana na kwamba walikuwa wanafanya kazi pamoja lakini ikifika ni kwa faida Bahati anachukua yote.

Bahati, Weezdom
Image: Weezdom (Facebook)

Msanii Weezdom hatimaye ameweka wazi kiini na mwanzo wa ugomvi wake na msanii Bahati ambaye pia ndiye aliyemshika mkono na kumleta kwenye mwanga wa muziki wa injili kipindi kile kabla wapate unafuu kwenye miziki ya kidunia.

Weezdom anasema kwamba tofauti zake na Bahati zipo tena kw asana na hili halimfanyi kupunguza heshima yake kwa msanii huyo kwani anamheshimu kama mkombozi wake ila hawawezi fanya kazi Pamoja kwa sababu tofauti tofauti.

Anasema kwamba Bahati ndiye alimfundisha kuacha muziki na kuanza kuwa meneja wake ila ikafika mahali yeye anapiga kazi kama meneja wa kazi za muziki wa Bahati ila mambo yakijipa vizuri Bahati anakula peke yake na kumtenga meneja wake – Weezdom.

“Tulishindwa kufanya kazi Pamoja kwa sababu mimi huwa mkweli sana. Inafaa tukipata tumepata, si eti tukipata umepata. Sasa hapo ndio nilihisi tunatafuta halafu baadae mimi sifaidiki. Nikaona wacha tu nijikaze kivyangu lakini namshukuru sana kwa chenye amewahi nifanyia kwa maisha yangu,” alisema Weezdom.

Alisema tofauti yao ilikuja tu kutokana na shughuli za kibiashara na si mambo ya kibinafsi kama ambavyo wengi wanahisi.