"Hatukucopy Mubaba ya Dian B", Weezdom atetea ngoma yake 'Wazae'

Muhtasari

• Weezdom akana madai ya kucopy mawazo na maudhui ya ngoma ya Diana B, 'mubaba' katika collabo mpya na Manzi wa TRM kwa jina 'Wazae'

Weezdom na mpenzi wake mpya
Manzi wa TRM, Weezdom Weezdom na mpenzi wake mpya
Image: instagram/weezdom

Weezdom na mwanasosholaiti Manzi wa TRM wamejipata pabaya baada ya mashabiki na wafuasi wa muziki wa humu nchini kuwachamba kwenye mitandao ya kijamii kwamba collabo yao mpya kwa jina ‘Wazae’ wameiga mawazo na mistari kutoka kwai le ya ‘Mubaba’ ya msanii Diana B.

Wakizindua ngoma hiyo rasmi katika stesheni moja ya redio ya humu nchini, Weezdom ametetea ngoma yao na kusema kwamba hakuiga ile ya Diana B ambazo zinakaribia kufanana pakubwa kwa maudhui.

“Watu wanasema tuliiga ngoma ya Diana B. mimi ni fan wa Diana, so mimi husikiza ngoma yenye anatoa. Nadhani siwezi mcopy kwa sababu mimi nimekuwa kwa muziki for long tangu 2014 na sikushinda Groove Awards through kucopy watu,” alijitetea Weezdom.

Weezdom pia aliwasuta wale wanaosema kwamba aliiga na kusema kwamba wazo na maudhui katika ngoma ya Diana B ni tofauti ya kile kinachoonekana katika ngoma yake na Manzi wa TRM, ‘Wazae’.

“Idea yake na yetu ni tofauti juu yeye amekuja na mubaba, mwenye ameimba na yeye amekuja na mumama. Mimi sijakuja na mumama, nimekuja kuongelea kijana like, mbona uko na mubaba?” alielezea tofauti Weezdom.

Vile vile msanii huyo wa kitambo wa injili alitolea mfano wa kuonesha kwamba hajacopy Diana B kwa kusema kwamba nyimbo ni nyingi ambazo zina maudhui na hata majina ya kumpenda Yesu na watu hawasemi zinafanana ama watunzi wameigana.

“Tukihesabu nyimbo zenye zinaitwa ‘Jesus, I Love You’ ni kama elfu, hauwezi sema walikopiana. Musically vitu hufanana lakini ideas hukuwa tofauti,” alisema Weezdom.