Baba Talisha avunja kimya baadhi ya tiktokers wakimhushisha na kifo cha Brian Chira

"Hadi anakuja kusema eti mimi ndio niliua Brian Chira, unaona. Mpaka nakuja kushtuka. Ni kama anafurahia kwa sababu anaona Baba Talisha ndio gumzo sasa hivi, hiyo ndio njia anaweza kupata views" alisema Baba T.

Muhtasari

• Mtu kama Truth Watchdog anajaribu kuniulizia mambo ya uwajibikiaji pesa, yeye mwenyewe hata hakuchanga hata shilingi.' alisema.

Baba Talisha
Baba Talisha
Image: Screengrab

Tiktoker Baba Talisha amevunja kimya chake baina ya muendelezo wa uvumi wa mjadala usioisha kuhusu kifo cha Brian Chira.

Licha ya kuwekwa wazi kwamba marehemu Brian Chira alifariki katika ajali ya barabarani, baadhi ya wanatiktok wamekuwa wakiibuka na dhana mbalimbali wakijaribu kutafuta sababu tofauti ya ajali ya barabarani.

Baadhi yao wamekuwa wakiibua madai kwamba Baba Talisha, tiktoker aliyekuwa katika mstari wa mbele kufanikisha safari ya mwisho ya Brian Chira, wakidai ndiye alihusika kaitka kifo chake.

Baba Talisha katika mazungumzo na Mungai Eve, alivunja kimya chake na kusema kwamba huyo anayeendeleza taarifa kama hizo za kupotosha akitaka kuweka wazi maelezo ya pesa alizochangisha kwa ajili ya mazishi ya Chira, huenda hata hakuhusika kaitka kutoa mchango hata senti.

“Watu wengi katika mitandao ya kijamii haswa TikTok, kila mtu ako na maoni yake. Kwa hiyo mimi nawaacha wagonganishe kwa maoni yao, wakisema tumekula pesa 8m, mimi nakubali tu. Wakiniita mwizi wa pesa za matanga, mimi nakubali tu. Mimi sina shida kabisa,” alisema.

“Mmi huwa sipendi kubishana na watu siku hizi, haswa watu wenye wanaongea, mtu kama Truth Watchdog anajaribu kuniulizia mambo ya uwajibikiaji pesa, yeye mwenyewe hata hakuchanga hata shilingi. Yeye amejikita Zaidi katika stori za sijui Chira aliuliwa, sijui alipigwa risasi. Si huo ushahidi wote, kuna ofisi za DCI, kuna vituo vya polisi.”

“Si apelike ushahidi kule aseme huyu mtu aliuliwa na mtu Fulani. Hadi anakuja kusema eti mimi ndio niliua Brian Chira, unaona. Mpaka nakuja kushtuka. Ni kama anafurahia kwa sababu anaona Baba Talisha ndio gumzo sasa hivi, hiyo ndio njia anaweza kupata views. Kila siku ana’host watu TikTok akiniongelelea akinitusi,” Baba Talisha alisema.