Atawasumbua sana! #MUBABA ya Diana B views 400K

Muhtasari

• Msanii chipukia Diana B  amezidi kufanya kweli kwenye mtandao wa YouTube baada ya ngoma yake mpya #MUBABA kutazamwa na watu laki nne chini ya saa ishirini na nne.

• Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Marua ametoa shukuran nyingi kwa mashabiki wake ambao wameaminia kazi yake na wanazidi kumpa sapoti katika wimbo wake mpya ambao umetoka baada ya kisanga cha akaunti yake kudukuliwa.

Diana Marua
Diana Marua
Image: hisani

Msanii chipukia Diana B  amezidi kufanya kweli kwenye mtandao wa YouTube baada ya ngoma yake mpya #MUBABA kutazamwa na watu laki nne chini ya saa ishirini na nne.

Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Marua ametoa shukuran nyingi kwa mashabiki wake ambao wameaminia kazi yake na wanazidi kumpa sapoti katika wimbo wake mpya ambao umetoka baada ya kisanga cha akaunti yake kudukuliwa.

Ngoma hii ambayo inazungumzia msichana ambaye anapenda maisha mazuri na kupotezea wanaume wasiokuwa na hela katika jamii imeibua hisia nyingi miongoni mwa mashabiki huku baadhi yao wakihisi kwamba anatoa wosia hasi kwa kina dada.

Ifahamike kwamba ngoma hii ni kolabo kati yake na msanii chipukizi, Vinny Flava ambaye amepewa mkataba kama msanii wa kwanza chini ya Diana B Entertainment.

Diana B anaonekana kuzidi kuachia kazi licha ya baadhi ya mashabiki kutoa cheche kwamba hana kipaji cha kuimba.

Msanii huyo pia amewashukuru Terrence Creative na Milly Chebby kwa kukubali kutokea kwenye ile video jambo ambalo anaamini pia limeweza kufanya ngoma hiyo kuwafikia mashabiki wengi.

Ifahamike kwamba ngoma ya mwisho aliyoiachia ilitazamwa na mashabiki milioni moja chini ya saa ishirini nan ne, huku wengi wakisubiri kuona ngoma hii ya #Mubaba itaweka rekodi gani.