Mimi ni tofauti, huwa sipendi 'sponsors' - Manzi wa TRM

Muhtasari

• Manzi wa TRM amekana madai ya kupenda 'masponsor' licha ya kusikika akiimba kwenye wimbo.

• Amesema pesa zake hutokana na biashara zake na hategemei 'sponsor' kukidhi mahitaji yake.

Instagram
Manzi wa TRM Instagram
Image: Carol Leehavi

Mwanasosholaiti na mfanyibiashara Manzi wa TRM amesema kwamba yeye ni tofauti kabisa na wanadada wengine kwani yeye hapendi kabisa kutegemea wanaume kwa pesa na hapendi kabisa kuwa na ‘sponsors’ ambao wengine wanawaita ‘wababaz’.

Akijibu madai hayo kwenye mahojiano ya stesheni moja ya redio nchini ambako aliulizwa kuhusu kipande fulani kwenye wimbo wake mpya alioshirikishwa na msanii Weezdom kwa jina ‘wazae’, Manzi wa TRM alijitetea na kusema kwamba huo ni wimbo tu na wala hamaanishi alichokiimba na kusema kwamba kipande hicho aliandikiwa na Weezdom ambaye pia amefichua ni mpenzi wake mpya.

Manzi wa TRM alijitetea kwamba yeye hategemei kupata kipato chake kutoka kwa ‘masponsors’ na kusema kwamba yeye hela zake huzipata kutoka kwa biashara zake. Pia alisema kwamba yeye taaluma aliyoisomea ni ya ubunifu katika ujenzi na biashara za real estate.

“Sijawahi tegemea mwanaume,” alisisitiza Manzi wa TRM.

Hili linaonekana kuenda kinyume na mistari katika kipande cha wimbo huo mpya ambao wameutoa Jumanne vambapo anasema kwamba anapenda wazee kwa sababu vijana hawana heshima.

“Mimi nataka wazae, vijana hawana heshima, hawana madooh, nataka wazae, wababaz,” sehemu ya kipande hicho inasema.

Weezdom alijitetea kwa kuandika kipande hicho na kusema kwamba ni mistari iliyoimizwa na matamshi ya awali ya Stacey Mylee kwamba alikuwa anatafakari kukubali ofay a kununuliwa gari ya Range Rover kutoka kwa ‘mubabaz’.