Weezdom aachia kibao kipya baada ya kimya kirefu

Muhtasari

• Baada ya kimya kirefu bila kutoa ngoma yoyote, hatimaye msanii Weezdom amerejea na kibao kipya ambacho amemeshirikisha Carol Leehavi.

• Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Weezdom amewaomba mashabiki wake kumpa sapoti kwa kutazama kibao hicho na kuwaahidi kwamba sasa amerejea kuchapa kazi.

Weezdom
Weezdom
Image: Hisani/Weezdom

Baada ya kimya kirefu bila kutoa ngoma yoyote, hatimaye msanii Weezdom amerejea na kibao kipya ambacho amemeshirikisha Carol Leehavi.

Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Weezdom amewaomba mashabiki wake kumpa sapoti kwa kutazama kibao hicho na kuwaahidi kwamba sasa amerejea kuchapa kazi.

‘’Baada ya kimya kirefu kwenye muziki, hatimaye nimerudi mashabiki wangu. Wimbo wangu mpya na Carol Leehavi tayari unapatikana katika mtandao wa Boomplay,” Weezdom aliandika.

Siku chache zilizopita Weezdom alimtambulisha rasmi Carol Leehavi kama mpenzi wake, huku mashabiki wakitoa hisia tofauti kuhusu hatua aliyoichukua msanii huyo.

Kwa sasa, kutokana na mtiririko wa matukio katika maisha ya Weezdom, washikadau wengi wanazidi kujiuliza iwapo msanii huyo alikuwa anatafuta kiki na binti huyo ili kusukuma muziki wake.

Katika siku za hivi karibuni, wasanii wengi wameonekana kutumia kiki kuhakikisha muziki wao unawafikia watu wengi na kwamba unafanya vizuri katika mitandao ya kijamii.