Weezdom amuonya Mylee Staicey kukoma kutumia jina lake

Weezdom
Weezdom
Image: Hisani/Weezdom

Msanii Weezdom amevunja kimya chake   kwa  kumuonya aliyekuwa mpenzi wake Mylee Staicey kuwa aache kutumia jina lake kutengeneza kiki ili ajulikane.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram alieleza kuwa Mylee hakubali kuwa  mahusiano yao yalifikia mwisho na hivyo kumtaka  aache kutumia jina lake kwenye mahojiano anayoshiriki.

Hii imewadia baada ya Mylee kutangaza wazi kujiunga na siasa za humu nchini, ambapo amekuwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuuza sera atakazofanyia eneo bunge la Kibwezi.

“Mwambieni Mylee Staicey kuwa Mungu alinipa uwezo wa kumjua. Na mimi niko na ushahidi wa kila kitu kuhusu mahusiano yangu na yeye, hivyo aache kutumia jina langu kutengeneza kiki, sitaki tuaibishane, namtakia kila la kheri,”alisema Weezdom.

Hapo awali, Mylee alikuwa ameeleza kuwa alikuwa ameonywa na rafiki yake kuhusu kuingia kwenye mahusiano na msanii huyo.