Mylee Staicey akiri kuonywa dhidi ya Weezdom

Muhtasari

•Mshawishi wa mitandao na mfanyabiashara,Mylee  Staicey amefunguka na kueleza kuwa Kilichosabisha mahusiano ya na mwimbaji wa injili Weezdom kufikia tama

•Alieleza kuwa alikuwa ameonywa  kuchumbiana na mwimbaji huyo lakini  licha   ya onyo zote hizo  ziliambulia patupu

Mylee Staicey
Mylee Staicey
Image: Hisani

Mshawishi wa mitandao na mfanyabiashara,Mylee  Staicey amefunguka na kueleza kuwa Kilichosabisha mahusiano yake na mwimbaji wa injili Weezdom kukatika.

Staicy Mylee ametangaza azma ya kuwania kiti cha ubunge cha Kibwezi kwenye uchaguzi ujao wa tarehe 9 Agosti.

Staicey   alianza kuwa mshawishi wa mitandao akiwa bado mwanafunzi,lakini hakuwa na matarajio ya kujulikana haraka kama ilivyotokea.

Kupitia mahojiano na kituo cha radio moja humu nchini alieleza kuwa walipatana na Weezdom kwenye hafla moja, Kaunti ya Kiambu ambapo alikuwa amepeleka rafiki yake.

Alieleza kuwa alikuwa ameonywa  kuchumbiana na mwimbaji huyo lakini   onyo  zote ziliambulia patupu, baada ya hapo alieleza Weezdom alimtamfuta kwenye ukurusa wa instagram na mapenzi yao  yakaanza kuota.

"Tulikutana wakati wa hafla moja huko Kiambu, rafiki yangu na Weezdom walijuana kwa hivyo utambulisho ulianza,”Alisema Mylee Staicey.

Vilevile, alieleza kama si mahusiano yake na Weezdom asingeweza  kutambulika humu nchini kwa kasi kama ilivyotokea.