Mimi ni Mkwe wa Taifa, Khadija Kopa asema

Muhtasari

• Mwanamuziki  wa nyimbo za Taraab kutoka nchi ya Tanzania, Khadija Kopa ameeleza kuwa yeye ni mkwe wa taifa

• Alisema kwa sasa popote anapotembea anaitwa mkwe wa taifa, kauli ambazo zinazofanya ajivunie kuwa mama wa Zuchu.

Khadija Kopa
Khadija Kopa
Image: Hisani

Staa wa Taraab kutoka nchi ya Tanzania, Khadija Kopa ameeleza kuwa yeye ni mkwe wa taifa.

Kauli hii imechukuliwa kwa uzito kuzingatia tetesi kwamba Diamond anatoka kimapenzi na mwanamuziki Zuchu.

Khadija Kopa ambaye alikuwa anahojiwa na kituo kimoja cha habari nchini  Tanzania, alisema kwamba furaha kubwa kwa kila mzazi, ni kuona watoto wake wakikua kwa madili  mema yanayofaa.

Alisema popote anapotembea anaitwa mkwe wa taifa, kauli ambazo zinazofanya ajivunie kuwa mama wa Zuchu.

"Umezaa Mtoto  wa kike utakosa aje kuitwa Mkwe, Mimi ni mkwe wa taifa, Nimefunza watoto wangu kwa njia inayofaa  kwa hivyo sina shaka kusema  anajua jinsi ya kutunza familia," alisema Khadija Kopa.

Khadija, ambaye ni mama wa mwanamuziki wa kike mashuhuri nchini Tanzania, Zuchu alisifia  binti yake akisema amemlea kwa  mila na desturi za kukaa kwenye ndoa hivyo hana shaka na maumuzi ya Mwanawe atakayofanya ifikiapo tarehe 14 mwezi huu.