Nipeni heshima zangu - S2kizzy

Muhtasari

• Mnipe heshima ninayostahili mkitaja jina langu, S2kizzy amewataka watu.

• Hii ni baada ya ngoma ya #Gidi, yake msanii Diamond ambayo ni mpya kabisa kuimbwa kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la Grammy Global Spin.

S2kizzy
Image: Instagram

Mzalishaji nguli wa muziki kutokea nchini Tanzania, S2kizzy amelichukua jukwaa la uzalishaji muziki kwa kimbunga baada ya ngoma alizozitayarisha za wasanii mbali mbali kufanya vizuri Zaidi kwenye majukwaa ya kimziki kote nchini.

Mzalishaji huyo S2kizzy ambaye amehusika katika kazi nyingi za msanii Diamond Platnumz amewataka watu kumkabidhi heshima yake la sivyo aichukue mwenyewe.

 Hii ni baada ya ngoma ya #Gidi, yake msanii Diamond ambayo ni mpya kabisa kuimbwa kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la Grammy Global Spin.

Mzalishaji huyo ametoa sababu Zaidi ni kwa nini anafaa kupewa heshima anazostahili kwa kusema kwamba kando na Gidi kuchezwa kwenye hafla ya Grammy, pia ngoma ya #Tetema ambayo msanii Rayvanny alimshirikisha Diamond ilikuwa ngoma ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kuchezwa katika jukwaa la MTV Europe.

Image: Screengrab (Instagram)

“GIDI ya @diamondplatnumz Nyimbo ya kwanza katika historia kuonyeshwa kwenye @recordingacademy

GRAMMY

TETEMA ya @rayvanny nyimbo ya kwanza kuruka katika maonyesho ya @mtv EUROPE

Zote zikiandaliwa na mimi na nyingine nyingi zinakuja

Mnipe heshima ninayostahili mkitaja jina langu” ameandika S2kizzy kwenye instastories zake