Diamond atumbuiza kwenye hafla ya Grammy

Muhtasari

• Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kabisa kuwahi kutokea kutoka Afrika mashariki kupata mwaliko rasmi wa kutumbuiza katika hafla maalum kwqa jina Grammy Global Spin.

Diamond Platnumz
Image: Facebook

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kabisa kuwahi kutokea kutoka Afrika mashariki kupata mwaliko rasmi wa kutumbuiza katika hafla maalum kwqa jina Grammy Global Spin.

Nguli huyo wa mitindo ya bongo fleva alitumbuiza katika show hiyo iliyopeperushwa moja kwa moja mubashara kupitia mtandao wa YouTube

Ni show ambayo iliasisiwa mwaka wa 2021 huku lengo lake kuu likiwa ni kuusukuma muziki wa Afrika kwenda ngazi za juu Zaidi

Image: Instagram

Kando na kuupatia muziki wa Afrika kipaumbele, show hiyo pia inalenga kusukuma miziki ya Latin.

Hii show ya Grammy Global Spin iliona mwanamuziki huyo akiimba wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza kabisa kwenye ukumbi huo. Kibao kipya ambapo watu wote ndio ilikuwa mara ya kwanza kukisikia kinakwenda kwa jina Gidi. Kibao chenyewe kina midundo ya ki Afro

 

Msanii huyo aliburudisha na vibao vyake vingi vilivyotamba na kufanya vizuri kwenye charts za Afrika Mahsariki na kwa kweli ulikuwa ni usiku wa kumbukumbu kwake.