Mume wa Zari, Shakib amuomba Harmonize mechi ya kupigana ngumi

“Zari unafahamu hili? Mume wako anajaribu kufanya mchezo na kifo,” Harmonize alimwambia Zari.

Muhtasari

• Kwa mshangao, Harmonize alimjibu akimwambia kwamba hajui anachocheza nacho, akisema kuwa laiti Shakib angelijua basi angelighairi ombi lake la kutaka kupigana naye.

Shakib amuomba Harmonize mechi
Shakib amuomba Harmonize mechi
Image: Instagram

Saa chache baada ya Harmonize kutangaza kujikita katika mazoezi ya kupigana ngumi ili kumenyana na bondia Hassan Mwakinyo na kuondokea tasnia ya muziki aliyoitaja kuwa na chuki nyingi, mume wa sosholaiti Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amemfuata na kumuomba pambano.

Shakib alikwenda kwenye DM ya Harmonize katika mtandao wa Instagram na kumjibu Harmonize kuwa ameamua kufanya mazozi tayari kuingia kwa mchezo wa ngumi.

Kijana huyo Mganda alimuomba Harmonize kukubali pambano lao liandaliwe nchini Tanzania, huku akisema kwamba kutokana na pambano hilo, watapata kutengeneza pesa ili kufanya kazi za kutoa misaada kwa watu wasio nacho kwenye jamii.

“Siku njema kwako kaka, ni vizuri katika hatua hii mpya ya mchezo wa ngumi. Ningependa kuwa na mchezo wa kupigana ngumi na wewe nchini Tanzania, tutatengeneza pesa kutokana na pambano letu ili kusaidia katika misaada, natumai nitapata jibu lako hivi karibuni,” Shakib alimwandikia.

Kwa mshangao, Harmonize alimjibu akimwambia kwamba hajui anachocheza nacho, akisema kuwa laiti Shakib angelijua basi angelighairi ombi lake la kutaka kupigana naye.

“Hebu tazama huyu kwanza, itakufanya ubadilishe nia yako,” Harmonize alimjibu.

 Pia, Harmonize alimtaka Zari kumkanya mumewe akisema kwamba atamuumiza vibaya ikiwa ataendelea na nia yake ya kutaka kuingia ulingoni na yeye.

“Zari unafahamu hili? Mume wako anajaribu kufanya mchezo na kifo,” Harmonize alimwambia Zari.

shakib harmonize
shakib harmonize

Awali, tuliripoti kwamba Harmonize na Zuchu walikuwa wakipararuana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu  ni nani mbabe katika muziki.

Zuchu alimwambia Harmonize kwamba amemzidi katika takwimu zote kenye mitandao ya kidijitali ya utiririshaji miziki, jambo lililomkwaza Harmonize na kutaka kuachia muziki ili kujitupa mazima kwenye mchezo wa ngumi.